Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


KATIBU MKUU WA SEKRETARIETI YA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Alhaji Muhammad Mumuni (kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Ubeligiji Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala baada ya kumaliza mazungumzo naye ofisini kwake Brussels. Alhaji Mumuni alifika ofisi za Ubalozi wa Tanzania kuishukuru Tanzania kwa kumuunga mkono toka alipoteuliwa miaka miwili iliyopita hadi anapomaliza kipindi chake cha miaka miaka miwili ya kutumikia Sekretarieti ya...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WA SEKRETARIETI YA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Afrika, Karibiani na Pacific, Balozi Patrick Gomes (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania katika Jumuiya ya Ulaya, Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada kumaliza kikao cha kushauriana masuala mbalimbali ofisini kwa Balozi Kamala Brussels. Kulia ni Balozi Jagne msaidizi wa Balozi Gomes.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ABAINISHA MTAZAMO MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA AFRIKA, KARIBIANI, PASIFIKI NA JUMUIYA YA ULAYA

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akihutubia wadau wa ushirikiano kati ya nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya. Balozi Kamala alisisitiza umuhimu wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya kushirikiana katika kujenga uchumi, kukuza na kutumia teknolojia kuharakisha maendeleo na kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara yenye kunufaisha pande zote. Wadau wa ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiongoza kikao cha 873 cha Kamati ya Mabalozi wa ACP. Kikao hicho kimefanyika Brussels kuandaa kikao cha Baraza la Mawaziri la ACP kitanachotarajiwa kufanyika Nairobi Kenya tarehe 16-20 Juni,2014.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ASHUKURU BENKI YA MAENDELEO YA ULAYA KWA MIKOPO NA MISAADA INAYOITOA KWA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akishukuru Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EIB) kwa kutoa  mikopo ya gharama nafuu na kusaidia Maendeleo ya nchi za ACP. Balozi Kamala ameitaka Benki hiyo kuongeza kiwango cha mikopo inayotoa katika nchi za ACP kutoka asilimia 10 ya mikopo inayotoa sasa hadi asilimia 20. 
Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP leo imekutana na Uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ulaya, Luxembourg...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA MASUALA YA MASUALA YA SIASA NA MAENDELEO YA JAMII WA SEKRETARIETI YA ACP

Balozi wa Tanzania BELUX, Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ACP anayesimamia masuala ya siasa na maendeleo ya jamii Mhe. Michele Dominique Raymond. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kukutana na viongozi mbalimbali wa Sekretarieti ya ACP Brussels kwa lengo la kuelewa vyema changamoto zinazokabili ACP na kubaini masuala kipaumbele wakati wa kipindi chake cha uenyekiti...

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA BARAZA LA NISHATI DUNIANI

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Nishati Duniani Bwana Selim Kuneralp (kushoto) na Mhandisi John F. Kitonga wa kitengo cha Maendeleo ya Nishati Wizara ya Nishati na Madini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bwana Kuneralp amefika ofisi za Ubalozi wa Tanzania Ubeligiji kubadilishana mawazo na Balozi Kamala kuhusu kazi za Baraza la Nishati Duniani na jinsi Tanzania inavyoweza...

 

10 years ago

Michuzi

balozi kamala akutana na katibu mkuu wa taasisi ya kusambaza umeme vijijini na Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Jiji la Oestende la Ubelgji

Balozi wa Tanzania Ubelgji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika  picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kusambaza Umeme Vijijini katika nchi  zinazoendelea Bwana. Marcus Wieman (katika). Bwana Wieman  alikutana na Balozi Kamala leo Brussels kumweleza mipango ya taasisi yake ya kusambaza umeme vijijini katika nchi zinazoendelea.Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu  Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Jiji la...

 

9 years ago

Michuzi

MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIKI WAMUAGA BALOZI DR. KAMALA

Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki Jumuiya ya Ulaya. Mabalozi hao wamemshukuru Balozi Kamala kwa kazi  aliyofanya ya kuongoza Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki. Balozi Kamala amemaliza kipindi chake cha kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA NAIBU KATIBU MKUU WA ACP ANAYESIMAMIA UTAWALA NA FEDHA

Balozi wa Tanzania BELUX, Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific(ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa ACP anayesimamia Utawala na Fedha Bi. Nthisana Phillips ofisini kwake Brussels. Balozi Kamala anaendelea na ziara ya kukutana na watendaji wakuu wa ACP kwa nia ya kubainisha masuala ya kupewa kipaumbele na ACP katika kipindi cha miezi sita ijayo.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani