KONA YA MAKENGEZA : Usanii si sanaa
Mimi ni msanii. Hapana, jamani, mimi siyo mtangazania, mtiania, mbwiania, mfiania, sina nia ya ya kuwania au kubania nia za wengine. Ni msanii mpenzi wa sanaa. Bahati mbaya nafasi zetu za sanaa zimevamiwa na makanjanja wa sanaa ambao wanajiita wanasiasa eti siasa ni usanii. Siasa si usanii halali ingawa siasa na sanaa mara nyingi wanalala kitanda kimoja.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mwananchi06 Jul
KONA YA MAKENGEZA :Makengeza juu, juu zaidi!
Kwanza kabisa, awali ya yote, nasimama kidete bila shukrani za dhati kupinga kwa nguvu zote jinsi gazeti lako lilivyonidhalilisha mimi pamoja na ng’wanamakengeza wenzangu. Yaani unaanza kutoa makala mfululizo kuhusu athari za makengeza hivihivi tu! Bila hata kutuuliza sisi na kupata maoni yetu? Bila kujali hisia zetu?
9 years ago
Mwananchi11 Oct
KONA YA MAKENGEZA : Umimi na Umeme
Mwishiwa mwenzangu,
Hebu nisaidie. Tangu matangazo ya juzi nawasikia watu:
‘Si ndio haohao. Ngoja tarehe 25. Watakoma kabla hawajakomaa.’
‘Naam. Za mhujumu hazifiki 40. 25 zinatosha.’
Kisha watu wanacheka. Kupanda daladala vilevile.
9 years ago
Mwananchi27 Sep
KONA YA MAKENGEZA : Nyomi ya matochi
Nimechoka kampeni. Nimechoka vijembe vya wanaojiita majembe huku wakilimana badala ya kuzingatia kilimo cha mahindi. Kumbe kilimo kwanza maana yake ni kutumia kiserema kuwachimbachimba wapinzani wako kwa udaku na uzushi.
9 years ago
Mwananchi18 Oct
KONA YA MAKENGEZA : Videmo watadumu?
Haya jamani, nadhani huyu mtafiti si wa kupuuzwa.
Nimegundua kwamba demokrasia au tuseme kidemo ni kama kifaru. Ni mnyama mkubwa, mwenye nguvu, ni mnyama anayependeza hadi kila mtu anataka kuona kidemo angalau mara moja katika maisha yake.
9 years ago
Mwananchi20 Dec
KONA YA MAKENGEZA: Elekezi, tekelezi au telekezi?
Naam. Ngoma ikipigwa, hata wengine waliosahau jinsi ya kucheza, ghafla wanaanza kutingisha. Waliopenda ngoma za nje wanakumbuka za ndani. Tehe tehe tehe. Yaani, kwa miaka mingi, tulicheza ngoma nyingine. Maana ya ziara ilieleweka kabisa. Ni kwenda kukagua maofisi, maduka, masoko ya nje kisha kurudi na vitu lukuki ili kuendelea kuvikagua nyumbani.
9 years ago
Mwananchi29 Nov
KONA YA MAKENGEZA : Sisimizi ndani ya sukari
Juzi sisi waishiwa tulikutana tena sebuleni mwetu. Kwa bahati nzuri, wale wasakasupu hawakuwepo. Baada ya Mwishiwa Supu kuamuru hakuna kupewa bakuli ya dezo zaidi ya moja, wachache walisusa eti. Bila bakuli tatu na minofu kibao hawako tayari kukaa na kujadili mambo muhimu ya taifa letu na waishiwa wenzetu.
9 years ago
Mwananchi22 Nov
KONA YA MAKENGEZA: Sera ileeeee sura hiiii
Juzi nilishangaa sana kuletewa barua:We Mwishiwa Makengeza,Watakiwa kuhudhuria bila kukosa kikao cha kwanza cha Waishiwa ndani ya Awamu ya Tano. Haki na masupusupu yatakuwapo kama kawaida.
9 years ago
Mwananchi06 Sep
KONA YA MAKENGEZA : Aliyezoea uchafu hawezi kuuzoa
Duh! Nazidi kupata barua za kila aina. Hebu soma hii hapa na unipe mawaidha,jana niliota. Niliota niko kijiji fulani na kulikuwa na vita.
10 years ago
Mwananchi22 Feb
KONA YA MAKENGEZA: Nisipokataa ukatili, na mimi mkatili
>Mara nyingine kejeli hazifai. Mara nyingine hata uandishi unaacha ladha mbaya mdomoni. Mara nyingine kukaa mbele ya kompyuta na kuandika huku watu wanateketea ni kama kukwepa majukumu. Mara nyingine ...
Top 10
Tanzania Today
Today Breaking News,Tanzania World News
13-February-2025 in Tanzania