Mtoto afa kwa kuzama bondeni
KARIM Ramadhan (15), mkazi wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekufa baada ya kuzama kwenye bonde la shamba la mpunga. Mtoto huyo alizama alipokuwa akicheza na wenzake, ambapo alikuwa akijaribu kuvua samaki kwenye bwawa hilo lililopo Magereza. Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alithibitisha tukio hilo. Alisema kabla ya kifo hicho, mtoto huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa.
habarileo
Magazeti ya Leo
Zinazosomwa Sasa
-
1
-
2
-
3
-
4
-
5
-
6
-
7
-
8
-
9
-
10