Mtoto albino aliyenyang'anywa mikononi mwa mamaye akutwa amekatwa miguu, mikono yote. Kiwiliwili chake chatelekezwa msituni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo.
Siku tatu baada ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Yohana Bahati (1), kutekwa na watu wasiofahamika, hatimaye mwili wake umepatikana ukiwa umekatwa miguu, mikono yote na kiwiliwili chake kufukiwa shambani katika Kitongoji cha Mapinduzi, Kijiji cha Rumasa ndani ya hifadhi ya msitu wa Biharamulo Wilaya ya Chato, mkoani Geita.
Mtoto huyo alinyakuliwa Jumapili iliyopita nyumbani kwao saa 2:15 usiku akiwa amebebwa na mama yake mzazi, Esther...
Vijimambo