Nyumba tisa zachomwa moto Z'bar Dk. Magufuli akitangazwa mshindi.
Nyumba tisa zimeteketezwa kwa moto katika kisiwa cha Tumbatu Kaskazini Unguja muda mfupi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza ushindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wafuasi na wanachama wa CCM kisiwani hapo walianza kushangilia ushindi huo. Hata hivyo, wakati wakiendelea kushangilia ushindi huo huku wakilidhihaki kundi lingine hali iliyosababisha warushiane...
Vijimambo