Polisi 'feki' wawili wafungwa miaka mitano
Mahakama ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, imewahukumu kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja, Joseph Christopher (25) mkazi wa kijiji cha Nkome na Bahati Juma (28) mkazi wa Katoro wilayani Chato, baada ya kuwatia hatiani katika shitaka la kujifanya maofisa wa polisi kwa lengo la kufanya utapeli.
Katika kesi hiyo, washitakiwa hao walidaiwa kufanya utapeli katika kijiji cha Buseresere, Septemba 4, mwaka jana na kujipatia simu mbili za mkononi pamoja na Sh. 11,000 taslimu kinyume cha...
Vijimambo