'Tofauti za dini zinatumika vibaya'
VIONGOZI wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wamesema tofauti za dini zao zimekuwa zikitumika vibaya kwa maslahi binafsi ikiwemo kisiasa na hivyo kusababisha migogoro. Wamesema licha ya kutumika kisiasa, pia tofauti hizo zinatumiwa vibaya kwenye uchumi, jamii na hata miongoni mwa watu binafsi jambo linaloleta migogoro kwenye jamii na kusababisha vifo, majeraha na uharibifu wa mali. Walitoa tamko hilo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mkutano wao wa siku nne wa amani.
habarileo
Top 10
Tanzania Today
Today Breaking News,Tanzania World News
13-February-2025 in Tanzania