UGANDA YALEGEZA MASHARTI YA 'LOCKDOWN', YATANGAZA KUVAA BARAKOA NI LAZIMA

Rais Yoweri Museveni ametangaza kuwa kuvaa barakoa ni jambo la lazima nchini humo kuanzia leo katika kipindi hiki ambacho marufuku ya kutotoka nje inalegezwa.
Hatua hiyo ilitangazwa Jumatatu usiku ambapo rais Museveni alihutubia taifa baada ya kumaliza siku 35 za marufuku ya kutotoka nje ama 'lockdown'.
Museveni amesema watu wanaweza kuvalia mpaka barakoa ambazo zimeshonwa kienyeji na vitambaa.
Hata hivyo, kumekuwa na mashaka kutoka kwa wataalamu wa afya juu ya ufnisi wa barakoa za kutengenezwa...
Michuzi