Ajali barabarani yaua wanafunzi 5
SIKU tatu baada ya kutokea ajali mkoani Lindi na Singida zilizogharimu maisha ya Watanzania 27, wakazi wa Mtwara nao wameingia katika majonzi baada ya gari dogo kupamia wanafunzi wa Sekondari ya Mustafa Sabodo, waliokuwa kwenye mchakamchaka na kuua watano.
habarileo
Habari Zinazoendana
10 years ago
Michuzi19 Mar
10 years ago
Michuzi13 Sep
SHAIRI: Ajali za barabarani
Ninalianza shairi, kwa majonzi ya dhahiri,Kwa kuwa tena si siri, ajali zimekithiri,Zaua kwa utitiri, hii sasa ni hatari,Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.
Nianze na madereva, kisha nimvae Kova,Unapokua dereva, tunahisi umeiva,Si mambo ya kujilevya, na kuua kina Eva,Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.
Umakini safarini, ndio nyenzo namba wani,Sheria barabarani, zifuate kwa makini,Sifa za vibarazani, hazina tija jamani!,Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.
Bosi...
11 years ago
Mtanzania31 Jul
Ajali yaua 19
Ajali ya basi la Morobest iliyotokea mkoani Dodoma
Debora Sanja, Dodoma na Fadhili Athumani, Mwanga
WATU 19 wamepoteza maisha na wengine 64 wamejeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro.
Habari kutoka mkoani Dodoma zinasema watu 17 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 2 asubuhi, katika eneo la Pandambili, lililoko Barabara ya Dodoma-Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari...
11 years ago
Tanzania Daima31 Mar
Ajali yaua 21
WATU 21 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Mkupuka, Kibiti, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Watu...
10 years ago
Habarileo16 Jun
Ajali yaua 23
WATU 23 wamekufa katika ajali iliyohusisha basi na lori mjini Mafinga, Iringa huku wengine 34 hali zao zikiwa mbaya.
10 years ago
Tanzania Daima09 Sep
Tuungane kudhibiti ajali za barabarani
TUMEKUWA tukiandika maoni kuitaka serikali kuchukua hatua kukomesha ajali za barabarani na tutaendelea kufanya hivyo hadi hapo tutakapoona hatua madhubuti zimechukuliwa kukabiliana na wimbi la ajali, ambazo kila mara zimepoteza...
11 years ago
Tanzania Daima09 Apr
Ajali za barabarani zaongezeka Iringa
TAKWIMU zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko la ajali za barabarani mara saba zaidi zinazohusisha pikipiki Mkoa wa Iringa kati ya Januari 1 hadi Machi 31 ikilinganishwa na miezi kama hii mwaka...
9 years ago
Habarileo14 Dec
Elimu yapunguza ajali barabarani
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema ajali za barabara zimepungua hadi 7,570 kwa kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka huu ikilinganishwa na ajali 13,466 zilizotokea kwa kipindi kama hicho mwaka jana.
11 years ago
Uhuru Newspaper16 Jun
Vigogo wahusishwa ajali za barabarani
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya vigogo nchini wanadaiwa kukwamisha mchakato wa kuzuia matumizi ya mabasi chakavu ya abiria, ambapo huingilia kati pindi sheria inapotaka kuchukua mkondo wake.
Pia, baadhi wamekuwa wakilazimisha askari wa usalama barabarani kutojaribu kuyakamata mabasi hayo, hatua inayodaiwa kukwamisha utendaji kazi wa askari.
Kwa mujibu wa sheria, magari yote yaliyochakaa hayaruhusiwi kubeba abiria ili kupunguza ajali ambazo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na uchakavu.
Mwanzoni mwa...