Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAENDELEO WA JUMUIYA YA ULAYA

Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo na Misaada wa Jumuiya ya Ulaya Mhe. Pierre Amilhat ( kushoto), Bi. Camilla Lombard Msaidizi wa Mhe Pierre (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji Mhe. Nyamtara Mukome (wa pili kulia). Mhe Pierre amekutana leo na Balozi Kamala ofisini kwake Brussels kumweleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na inayopangwa...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge hao wanashiriki ziara ya mafunzo Brussels ya kutembelea taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Ulaya.

 

11 years ago

Michuzi

MKURUGENZI WA SEKRETARIETI YA DUNIA YA NISHATI AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Dunia ya Nishati Bwana. Steivan Defilla (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada ya kumaliza kikao ofisini kwake. Kulia ni Bwana. Nodal Tayel Mratibu wa Taasisi hiyo. Ujumbe huo ulifika Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Brussels kueleza faida za nchi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Nishati Duniani.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI WA AFRIKA WA KAMPUNI YA TE (TE Connectivity)

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya TE (TE Connectivity) Bi. Patricia Testa kitabu kinachobainisha fursa za uwekezaji Tanzania. Bi. Patricia amemtembelea Balozi Kamala leo Ofisi kwake Brussels kumweleza mipango ya kampuni yake kuingia katika soko la Tanzania. Pamoja na mambo mengine Balozi Kamala ameishauri kampuni hiyo kushiriki ziara ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Ubelgiji itakayofanyika Tanzania mwezi Novemba...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MBUNGE KIJANA WA BUNGE LA ULAYA

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mhe. Victor Negrescu Mbunge wa Bunge Ulaya vitabu vya kuitangaza Tanzania. Mhe. Negrescu ni kati ya wabunge vijana sabini wa Bunge la Ulaya na leo hii alimtembelea Balozi Kamala ofisini kwake Brussels.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA DELANOUT YA UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akimkabidhi zawadi ya mwamvuli unaotangaza vivutio vya Utalii Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DELANOUT ya Ubelgiji Bwana. Jackson Delanout. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kuhamasisha makampuni ya Ubelgiji kushiriki kwenye ziara ya biashara ya makampuni ya Ubelgiji  itakayofanyika Tanzania, Novemba mwaka huu.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ABAINISHA MTAZAMO MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA AFRIKA, KARIBIANI, PASIFIKI NA JUMUIYA YA ULAYA

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akihutubia wadau wa ushirikiano kati ya nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya. Balozi Kamala alisisitiza umuhimu wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya kushirikiana katika kujenga uchumi, kukuza na kutumia teknolojia kuharakisha maendeleo na kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara yenye kunufaisha pande zote. Wadau wa ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AWAAGA MABALOZI WALIOMALIZA KIPINDI CHA KUWAKILISHA NCHI ZAO JUMUIYA YA ULAYA

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) akimkabidhi zawadi Balozi wa Togo Jumuiya ya Ulaya Balozi Kodjo Sagbo kwa niaba ya Kamati ya Mabalozi wa ACP. Balozi wa Togo amemaliza kipindi chake cha kuwakilisha nchi yake Jumuiya ya Ulaya. Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa kwanza kutoka kulia) akiwa katika picha...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA USALAMA WA CHAKULA YA UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Chakula ya Ubelgiji Bwana. Pierre Nassens ( wa pili kutoka kushoto). Balozi Kamala ametembelea taasisi hiyo leo Brussels kushauriana nayo  jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania. Wengine katika picha ni wataalamu katika taasisi hiyo.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA YA BRUSSELS

Balozi wa Tanzania Belux na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji na Biashara ya Brussels Bi. Benedicte Wilders (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa wa taasisi hiyo Bwana. Philip Feytons. Balozi Kamala amekutana na viongozi hao leo hii Brussels kuwaomba wahimize makampuni ya Brussels kushiriki ziara ya kibiashara inayoandaliwa kufanyanyika Tanzania mwishoni mwa mwaka huu.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani