BASHUNGWA AWAELEKEZA WAMILIKI WA VIWANDA KUZALISHA VIFAA KINGA VYA KUTOSHA KUKABILIANA NA CORONA.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Innocent Bashungwa Pamoja na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wameendesha Kikao cha Wadau kujadili upatikanaji na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kujikinga na COVID – 19 leo tarehe 13.05.2020 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua teknolojia na uzalishaji wa vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo....
Michuzi
Habari Zinazoendana
5 years ago
MichuziWAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUZALISHA VIFAA KINGA KUKABILIANA NA CORONA
Wazalishaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba wakionesha nguo ya kujikinga ambayo itaanza kutengeneza na baadhi ya viwanda nchini.
Waziri Ummy Mwalimu na Waziri Innocent Bashungwa wakiwa kwenye kikao na Umoja wa wazalishaji wa Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba wakati wa mkutano huo
Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na Umoja wa Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini wakati wa kikao cha kujadili namna ya uzalishaji wa vifaa kinga vya kukabiliana na...
5 years ago
MichuziMAT,SHIRIKA LA UTAFITI HPON WACHANGIA WA VIFAA VYA MILIONI 4.5 KINGA KUKABILIANA NA CORONA SHINYANGA
Chama Cha Madaktari Tanzania (Medical Association of Tanzania – MAT) na Shirika la Utafiti HPON (Heath For A Prosperous Nation) wametoa msaada wa Vifaa Kinga vyenye thamani ya shilingi Milioni 4.5 kwa ajili ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID -19) katika mkoa wa Shinyanga.
Vifaa kinga hivyo ambavyo vitatumika katika vituo vya kutolea huduma za afya mkoani Shinyanga vimekabidhiwa na wadau hao wa sekta ya afya leo Ijumaa Mei 22,2020 kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga...
5 years ago
MichuziBashungwa:Serikali kulinda Viwanda vinavyozalisha vifaa tiba ya kujikinga na Corona
5 years ago
MichuziSERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA KINGA KUKABILIANA NA CORONA (COVID-19)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke wakitia sahihi makubaliano ya kupokea msaada wa vifaa kinga vya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona. ********************************Na.WAMJW-Dar es Salaam
Ubalozi wa China nchini Tanzania umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi kuendelea kushirikian...
5 years ago
BBCSwahili06 Mar
Coronavirus: White House yakiri Marekani haina vifaa vya kutosha vya kupima virusi vya corona
5 years ago
BBCSwahili08 May
Virusi vya corona: Wanafunzi Kenya watengeneza vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona
5 years ago
MichuziKATAVI YAPOKEA VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA
* RC KATAVI ATOA SAA 48 KWA MCHINA ALIYEKATAA KUNAWA AFIKISHWE MAHAKAMANI.
Serikali Mkoani Katavi imepokea Vifaa tiba kwa ajili ya kuendelea na mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona ikiwemo vifaa vinavyotumika kupima joto la mwili ambapo ni miongoni mwa changamoto iliyokuwa ikiukabiri Mkoa huo huku Mkuu wa Mkoa wa Katavi akitoa masaa 48 kwa Jeshi la Polisi kumfikisha Mahakamani Raia wa Kichina aliyekataa kunawa mikono yake maji tiririka.
Akipokea Vifaa hivyo kutoka Water Reed Program...
5 years ago
MichuziSHIA ITHNA ASHERIA MWANZA WAKABIDHI VIFAA KINGA VYA CORONA JESHI LA POLISI
NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza
WAUMINI wa madhehebu ya Khoja Shia Ithna Asheria, jijini Mwanza wamejitosa kwenye mapambano ya vita dhidi ya Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Kirusi cha Corona (Covid-19) kwa kutoa msaada wa vifaa kinga vya ugonjwa huo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza.
Vifaa kinga hivyo barakoa 300, vitakasa mikono 500 na chupa 500 za sanitizer vilikabidhiwa juzi kwa Ofisa Mnadhimu wa jeshi hilo mkoani humu, Safia Jongo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza...
5 years ago
MichuziKAMPUNI YA QWIHAYA YAUNGA MKONO SERIKALI VIFAA KINGA VYA CORONA STENDI YA MAFINGA
Kipima joto kilichotolewa na Kampuni ya Qwihaya General Enterprises Co Ltd kimesababisha wananchi wanaofanya kazi stendi ya Mafinga wilayani Mufindi kusimamisha shughuli zao kwa muda ili wapime joto la miili yao.
Wananchi hao wakiwepo wapiga debe na wafanyabiashara ndogo ndogo walimteua mwenzao, akajifunza kukitumia na baadae walipanga foleni ili kila mmoja apime kujua joto la mwili wake.
Kifaa hicho, matenki mawili ya kuhifadhia maji na vitakasa mikono ni miongoni mwa...