Basi la Takbir laua watu 12
NA SEIF TAKAZA, IRAMBA
WATU 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine 19 kujeruhiwa, baada ya basi la Kampuni ya Takbir kugongana na lori la mafuta katika Kijiji cha Kizonzo, Shelui Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 1.30 usiku wakati basi hilo lilipokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Geita.
Alisema...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
10 years ago
Habarileo09 Sep
Basi laua watu 4 korongoni
AJALI nyingine imetokea nchini na safari hii imehusisha basi la Air Bus, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Tabora.
11 years ago
Habarileo15 May
Basi laua watu 10 Mwanza
WATU 10 wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria walilokuwa wakisafiria kugonga lori lililokuwa na kokoto lililoegeshwa kando ya barabara kisha kupinduka katika eneo la Nyamhongholo, jijini Mwanza.
11 years ago
Habarileo30 Apr
Basi laua watu 18 wakimsitiri marehemu
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika.
10 years ago
Habarileo21 Aug
Bomu laua watu 3 kwenye basi
WATU watatu wamekufa na wengine sita kujeruhiwa na bomu la kurusha kwa mkono lililotupwa kwenye gari la abiria na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wilayani Buhigwe, katika Mkoa wa Kigoma.
11 years ago
Habarileo13 Dec
Basi laua watu 12 papo hapo
WATU 12 wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Korogwe, Tanga kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Ajali hiyo ilitokea jana saa 1.30 asubuhi kwenye barabara kuu ya Segera-Chalinze katika kijiji cha Kwalaguru kata ya Kwedizinga wilayani hapa.
11 years ago
Michuzi30 Apr
BASI LA SUMRY LAUA WATU 1( WAKATI WAKISITIRI MAITI ILIYOGONGWA NA GARI SINGIDA.
![](https://ci3.googleusercontent.com/proxy/zSaPxWsKXfQnP_rz2cFLYndr134Dze4FNZsmYL6Nv3mndXZwS2NMYLv-SGEDJlBvl9NhHS1U3ryBQX_DQ5mFQVw7dmr7Uu6UlPDX4137x1YabIcpC82RJQ=s0-d-e1-ft#http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/sumry_300_183.jpg)
WATU 19 wakiwemo askari Polisi wanne wamepota maisha katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa...
11 years ago
Habarileo02 Feb
Basi laua polisi 5
ASKARI Polisi watano wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wamekufa papo hapo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso wa uso na basi la Kampuni ya Mohammed Trans. Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Corolla lenye namba ya usajili T 770 ABT lililotumiwa na polisi hao na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 997 AVW, mali ya Kampuni ya Mohammed Trans lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Dodoma.
10 years ago
Habarileo23 Apr
Ajali zarudi, basi laua 10
SIKU sita tangu ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace kuua watu 19 mkoani Mbeya, nchi imeendelea kukumbwa na ajali za barabarani. Safari hii watu kumi wamekatishwa uhai, kutokana na ajali ya basi na lori, iliyotokea mkoani Shinyanga jana.
11 years ago
Mwananchi06 Feb
Basi laua wawili, kujeruhi 40