Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Chenge, Tibaijuka, Ngeleja kikaangoni leo

mnglFredy Azzah na Shabani Matutu, Dar es Salaam
KAMATI Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Philip Mangula, leo inawahoji makada wa chama hicho waliopokea mgawo wa fedha za Escrow.
Makada ambao watawekwa kikaangoni kutokana na kupokea mgawo huo, ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Wiliam Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.
Uamuzi huo...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Habarileo

Tibaijuka, Chenge, Ngeleja wafungiwa vikao vya chama

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye KAMATI Kuu ya CCM (CC) imewasimamisha uongozi wa vikao vya chama, vigogo watatu wa chama hicho, akiwemo Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na kuhusishwa na sakata la Escrow.

 

10 years ago

Vijimambo

Kina Chenge, Tibaijuka kula kibano Escrow leo.

Wiki hii inatarajiwa kuwa ngumu kwa wanufaika wa mgawo wa uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow, wakati Baraza la Maadili litakapowaweka kikaangoni watuhumiwa kadhaa, wakiwamo, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.

Kwa mujibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili, litaanza vikao vya kuwahoji watuhumiwa mbalimbali kwa wiki tatu mfululizo jijini Dar es Salaam kuanzia leo.

Watuhumiwa wengine wa Escrow ambao watawekwa kitimoto ni...

 

10 years ago

Habarileo

Ngeleja awekwa kikaangoni Dar

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja akiwa na Mwanasheria wake Douglas Mmari wakati wakiingia kwenye Baraza la Maadili, Dar se Salaam jana.MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja, amekiri mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwamba, aliomba na kupokea Sh milioni 40.4, kutoka kwa James Rugemalira kwa kujitetea, alifanya hivyo kama ilivyo kawaida pia kwa wabunge wengine.

 

10 years ago

Mtanzania

Baraza la Maadili kumweka kikaangoni Ngeleja

willium NgelejaAziza Masoud na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
BARAZA la Maadili ya Utumishi wa Umma jana liliahirisha shughuli za kumhoji Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma, baada ya eneo la mahojiano, Ukumbi wa Karimjee kutumika kwa shughuli za kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba.
Kutokana na hali hiyo, baraza hilo litaendelea na shughuli zake leo ambapo Mujunangoma atahojiwa kutokana na tuhuma za kupokea...

 

10 years ago

Mwananchi

Ngeleja,Chenge wapelekwa Maadili

Licha ya Bunge kuazimia kuwa wenyeviti wa kamati zake waliotajwa kuhusika kwenye kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wavuliwe nyadhifa zao, hali imekuwa tofauti katika vikao vya kamati hizo vilivyoanza jana baada ya baadhi yao kuongoza vikao hivyo. Jana, Kamati Kuu ya CCM imeamua viongozi hao, Andrew Chenge, William Ngeleja Na Profesa Anna Tibaijuka wafikishwe Kamati ya Maadili ya chama.

 

10 years ago

Mwananchi

Makinda: Siwatambui Chenge, Ngeleja

Spika wa Bunge, Anne Makinda amesema hawatambui wenyeviti wa kamati tatu za kudumu za Bunge ambao Bunge liliazimia wavuliwe nyadhifa zao kutokana na kutajwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow.

 

10 years ago

Mwananchi

Wiki ngumu kwa Ngeleja, Chenge

 Hii ni wiki ngumu kwa wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge ambao wanatakiwa kuachia nafasi za uongozi kutokana na kuhusika katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ya Sh306 bilioni.

 

10 years ago

Habarileo

Chenge na Ngeleja waachia vyeo bungeni

Andrew ChengeWENYEVITI wa Kamati za Kudumu za Bunge, waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, wamejiuzulu nyadhifa zao.

 

10 years ago

Mtanzania

Spika awaandikia barua Chenge, Ngeleja

Anne Makinda

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda

NA AGATHA CHARLES
KUTOKANA na kile kilichoonekana kama kugoma kufanya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge ambazo wenyeviti wao wamehusishwa na fedha za Escrow kwa kutaka kwanza mwongozo wa Spika, Kamati hizo zimeagizwa kufanya uchaguzi huo kabla ya kuanza Mkutano wa Bunge Jumanne wiki ijayo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alisema tayari hadi jana Spika wa...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani