Kina Chenge, Tibaijuka kula kibano Escrow leo.
Wiki hii inatarajiwa kuwa ngumu kwa wanufaika wa mgawo wa uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow, wakati Baraza la Maadili litakapowaweka kikaangoni watuhumiwa kadhaa, wakiwamo, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Kwa mujibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili, litaanza vikao vya kuwahoji watuhumiwa mbalimbali kwa wiki tatu mfululizo jijini Dar es Salaam kuanzia leo.
Watuhumiwa wengine wa Escrow ambao watawekwa kitimoto ni...
Vijimambo
Habari Zinazoendana
10 years ago
Vijimambo04 Mar
Ngeleja ajimaliza Escrow, Adai hajapokea mgawo peke yake, Naye kigogo Ikulu kula kibano leo.
Ngeleja (47), ambaye amewahi pia...
10 years ago
Vijimambo08 Jan
Tibaijuka, Chenge watumiwa ankara kodi ya Escrow
Serikali imesema imeshachukua hatua za kulipwa kodi kutoka kwa watu walionufaika na mgawo wa fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema wizara yake imeshawaandikia ankara za malipo ya kodi wadaiwa wote waliopokea mgawo huo.
Nchemba, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), alisema serikali imewapatia siku 30 watu hao ili...
10 years ago
Mtanzania19 Jan
Chenge, Tibaijuka, Ngeleja kikaangoni leo
Fredy Azzah na Shabani Matutu, Dar es Salaam
KAMATI Ndogo ya Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Philip Mangula, leo inawahoji makada wa chama hicho waliopokea mgawo wa fedha za Escrow.
Makada ambao watawekwa kikaangoni kutokana na kupokea mgawo huo, ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Wiliam Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge.
Uamuzi huo...
10 years ago
Vijimambo27 Feb
Tibaijuka ala kibano, bado Ngeleja.
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka, alikumbana na ‘kibano’ mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya kusomewa mashtaka matatu na baraza hilo, likiwamo la kuomba fedha katika Kampuni ya VIP Consultant, inayomilikiwa na James Rugemalira, kinyume cha maadili ya viongozi wa umma.
Mashtaka mengine yanayomkabili Prof. Tibaijuka, ambaye alivuliwa Uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Rais Jakaya Kikwete...
10 years ago
Habarileo28 Jan
Chenge, Tibaijuka kuwekwa kitimoto
TUME ya Maadili ya Viongozi wa Umma itawaweka kiti moto watuhumiwa 9 ambao ni viongozi wanaohusishwa na kashfa ya uchotwaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
10 years ago
Mwananchi17 Jan
Kamati za Bunge zawagwaya kina Chenge, Ngeleja
10 years ago
Mtanzania08 Jan
TRA yatua kwa Chenge, Tibaijuka
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetua kwa vigogo waliopata mgawo wa fedha za Escrow na kuwataka kulipa kodi ya mapato kwa mujibu wa sheria.
Maofisa wa mamlaka hiyo walikwenda kwa vigogo hao na kuwasilisha mahesabu ya kodi walizochukua Januari Mosi mwaka huu ambapo kila aliyepata mgawo huo ametakiwa kulipa fedha hizo kabla ya Januari 30.
Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema msimamo wa...
10 years ago
Habarileo24 Feb
Wiki ngumu kwa Chenge, Tibaijuka
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kesho atasimama mbele ya Baraza la Maadili kujibu tuhuma za kukiuka maadili ya uongozi na kujipatia Sh bilioni 1.6 ambazo aligawiwa kutoka katika fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.
10 years ago
Mwananchi27 Nov
Chenge, Tibaijuka, Kilaini walipuliwa mabilioni ya IPTL