Fedha za IPTL kaa la moto
>Tuhuma za ufisadi wa zaidi ya Sh200 bilioni katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonekana kuwa kaa la moto na jana zilitikisa Bunge na kuibua mvutano mkali.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
Uhuru Newspaper13 Nov
Escrow kaa la moto
NA THEODOS MGOMBA, DODOMA KASHFA ya madai ya kuchotwa mabilioni ya shilingi kwenye akaunti ya ESCROW, imezidi kuwa moto kutokana na kuibua mjadala mkali bungeni kila kukicha. Tayari serikali iliagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo malipo hayo kwa Kampuni ya PAP, iliyonunua IPTL, yalifanyika kihalali, ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imepewa jukumu hilo. Hata hivyo, habari za kuaminika...
11 years ago
Tanzania Daima27 Feb
Posho kaa la moto bungeni
KINARA wa kudai nyongeza za posho kwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Richard Ndassa, jana aliwashambulia waandishi wa habari kwa kuandika habari zinazowagombanisha na wananchi. Alisema vyombo hivyo vinalitumia...
11 years ago
Habarileo17 Jun
Bajeti kaa la moto bungeni
KAMATI ya Kudumu ya Bajeti imeonesha wasiwasi kuhusu ongezeko la haraka la deni la taifa na kusema hali hiyo inatishia ukuaji endelevu wa uchumi. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Andrew Chenge aliliambia Bunge jana, ongezeko la ghafla la deni la taifa kutoka Sh trilioni 23.67 Machi mwaka jana, hadi Sh trilioni 30.56 Machi, mwaka huu, linadhihirisha wasiwasi wa matumizi mabaya ya fedha za umma.
11 years ago
Mwananchi21 Feb
Katiba Simba kaa la moto
9 years ago
Raia Tanzania07 Sep
Ubunge Arusha kaa la moto
HARAKATI za uchaguzi zimeanza rasmi katika Jimbo la Arusha Mjini baada ya vyama vikubwa viwili vyenye ushindani; Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzindua rasmi kampeni zao mwishoni mwa wiki.
Katika uzinduzi wa kampeni hizo, kwa mara nyingine wapiga kura walishuhudia ahadi lukuki zikitolewa na wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa vyama vyote viwili ambazo zimekuwa zikitekelezwa nusu nusu au zisitekelezwe kabisa.
Hata hivyo, ushindani wa...
10 years ago
Mtanzania27 Aug
Posho za Bunge kaa la moto
![Bunge](http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/08/Bunge.jpg)
Bunge
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
OFISI ya Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, imetoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu kuchelewa kwa malipo ya posho za wajumbe wa Bunge hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Habari na Itifaki wa Bunge Maalumu, Jossey Mwakasiyuka, alisema ofisi ya Bunge hilo imekerwa na baadhi ya vyombo vya habari kuchapisha taarifa hizo.
Alisema taarifa hizo ni za upotoshaji na zina lengo la kuwadhalilisha...
9 years ago
Mtanzania17 Nov
Unaibu Spika kaa la moto
>Jenister Mhagama ajitosa kumvaa Dk. Tulia Akson
>Wabunge washtukia figisufigisu ya mgombea kubebwa
>Ndugai apita bila kupingwa, Ukawa wamteua Medeye
NA WAANDISHI WETU, DODOMA
BAADA ya jana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumpitisha aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la 10, Job Ndugai, kuwania kiti cha uspika, vita kubwa inaonekana kuanza katika nafasi ya Naibu Spika.
Taarifa zilizopatikana jana mjini hapa, zinasema kuwa katika nafasi hiyo, baadhi ya vigogo wa Serikali wanataka Dk. Tulia...
11 years ago
Habarileo29 Apr
Sheria Mabadiliko ya Katiba kaa la moto
HOFU ya kutopatikana kwa Katiba mpya, baada ya changamoto zilizojitokeza wakati wa awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu la Katiba, sasa ni dhahiri. Hofu hiyo inaonekana katika mahojiano maalumu kati ya waandishi wa gazeti hili na Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad.
9 years ago
Mtanzania13 Nov
Kufutwa uchaguzi Z’bar kaa la moto
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
UAMUZI wa Serikali wa kutoa tamko la kufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar umezua maswali kwa wananchi, huku Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (Zanzibar Law Society), Awadh Ali Said, akisema suala hilo ni la aibu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Amesema hatua ya kushindwa kuainisha vifungu vya Katiba ya Zanzibar kuhusu kufutwa kwa matokeo kwa tamko la mwenyekiti kwa kutaja vifungu vya kisheria visivyohusika ni wazi Serikali imeshikwa pabaya.
Awadh aliyasema hayo...