Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Fedha za kuchukulia fomu CCM ningezifanyia haya

Kwa mara ya kwanza Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetuacha hoi Watanzania kufuatia kujitokeza kwa makada wengi wanaowania kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

wanaCCM mkoani Tabora wamchangia mh. Lowassa fedha za kuchukulia fomu ya kuwania Urais

Mzee wa CCM wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Yusuf Bundala Kasubi, (kulia), akimkabidhi Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, zaidi ya shilingi milioni moja, zilizochangwa na wanachama wa CCM mkoani Tabora, ili azitumia kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwania urais kupitia chama hicho. Hafla ya kukabidhi fedha hizo ilifanyika nyumbani kwa Mtangaza nia huyo, mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 4, 2015. Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM wilaya ya Nzega mkoani Tabora,...

 

10 years ago

Dewji Blog

Lowassa achangiwa fedha za kuchukua fomu na Wana CCM mkoa wa Tabora

Mzee wa CCM wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Yusuf Bundala Kasubi, (kulia) akimkabidhi Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa,  zaidi ya shilingi milioni moja, zilizochangwa na wanachama wa CCM mkoani Tabora, ili kumuwezesha mtangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ili azitumia kulipia ada ya kuchukua fomu za kuwani urais kupitia chama hicho.

Hafla ya kukabidhi fedha hizo ilifanyika nyumbani kwa Mtangaza nia huyo, mjini Dodoma...

 

10 years ago

Michuzi

MH. MAKALLA ACHANGIWA FEDHA ZA KUCHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MVOMERO

Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla Aprili 3,2015 alichangiwa fedha kiasi cha sh 2,319,500 na wananchi wa kijiji cha Manyinga na vijiji vya jirani kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge mara muda utakapofika.
Tukio la kuchangiwa fedha za kuchukulia fomu lilichagizwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe aliyefanya ziara ya kukagua hospitali teule ya Bwagala na kisha kuongea na wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.
Alipopanda jukwaani, Dk. Stephen Kebwe...

 

5 years ago

CCM Blog

WAZIRI WA ZAMANI WA FEDHA ZANZIBAR, ACHUKUA FOMU ZA KUOMBA KUGOMBEA URAIS


Aliyekuwa Waziri wa Fedha na mipango Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohammed amekuwa mgombea wa 15 kujitokeza kuchukua Fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM.

 

10 years ago

Michuzi

Makalla aendelea kuchangiwa fedha za kuchukua fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Mvomero

Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameendelea kuchangiwa fedha za kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo hilo pamoja na kufanya kampeni na makundi mbalimbali wilaya ya Mvomero, na safari hii ni umoja wa wanawake wa CCM (UWT) tawi la madizini na kushirikisha matawi kumi kata ya Mtibwa na kata ya Diongoya.
Katika mkutano mkubwa wa kihistoria wanawake wa matawi walimtaka mbunge huyo wakati ukifika achukue fomu na wao wanamuahidi ushindi ndani ya chama na nje ya...

 

10 years ago

Michuzi

Maalim Seif Sharif achangiwa fedha za kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais wa zanzibar wakati utakapofika

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad,akipokea fedha taslim kiasi cha shilingi milioni mbili na laki tano, kutoka kwa Mwenyekiti wa CUF zoni ya Mjini Unguja, Massoud Khamis, ili aweze kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanzibar wakati utakapofika.Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akionyesha fedha alizokabidhiwa kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais. Mwenyekiti wa CUF zoni ya Mjini Unguja, Massoud Khamis, akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama hicho...

 

5 years ago

Michuzi

DKT.MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM...WANA CCM WAIMBA 'MAGUFULI BABA LAOO'


Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
RAIS Dk.John Magufuli amechukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) leo Juni 17,mwaka 2020 katika Makao ya Chama hicho Jijini Dodoma.
Dk.Magufuli anachukua fomu hiyo kwa ajili ya kuomba tena ridhaa ya kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM ikiwa ni awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya miaka mitano iliyoanzia mwaka 2015 mpaka mwaka 2020.Uchuguzi Mkuu mwaka huu unatarajia kufanyika...

 

10 years ago

Habarileo

6 tu warudisha fomu za urais CCM

Makao Makuu ya CCM mjini DodomaWIKI moja kabla ya kwisha kwa muda warudisha fomu kwa makada wa CCM waliojitokeza kuwania kupitishwa na chama hicho kuwania urais wa Tanzania, ni wanachama sita tu kati ya 39 ndio waliorudisha fomu mpaka sasa.

 

10 years ago

Habarileo

Fomu za ubunge, udiwani CCM leo

Makao Makuu ya CCM mjini DodomaBAADA ya mchuano wa kuwania uteuzi wa kugombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM uliomalizika kwa Dk John Magufuli kuibuka mshindi, kwa wiki moja kuanzia leo joto la siasa linatarajiwa kuhamia kwa makada wa chama hicho wanaowania kuteuliwa kuwania ubunge na udiwani kote nchini.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani