Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


KAMATI ZA TROIKA ZA MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI, PACIFIC NA JUMUIYA YA ULAYA ZAKUTANA

 Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa   kamati za Troika za Mabalozi wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kamati hizo zimekutana leo Brussels kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kulia kwa Balozi Kamala, ni Balozi Mhe. Dimitrious Touloupas Mwenyekiti wa Mabalozi wa...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKABIDHIWA UENYEKITI WA KAMATI YA MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC (ACP)

  Balozi wa Tanzania  Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya  ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Samoa Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya Mhe. Balozi Dr. Luteru  aliyemaliza kipindi chake cha uenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP. Balozi Luteru amemkabidhi Balozi Kamala uenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP leo, Brussels.

 

11 years ago

Michuzi

MHE MWIGULU MCHEMBA ASHIRIKI KIKAO CHA BUNGE LA PAMOJA LA AFRIKA, KARIBIANI, PACIFIC NA JUMUIYA YA ULAYA

Naibu Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Mchemba akifuatilia (kulia) kwa karibu kikao cha Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani, Pacific na Jumuiya ya Ulaya kinachoendelea Strasbourg Ufaransa. Mhe. Mchemba anawakilisha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific katika kikao hiki. Pamoja na mambo mengine, kesho atalihutubia Bunge na kujibu maswali ya Wabunge. Kulia ni Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

 

11 years ago

Michuzi

MHE OLUSEGUN OBASANJO AONGOZA KIKAO KAMATI YA WATU MASHUHURI YA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC (ACP)

Rais Mstaafu wa Nigeria na Mwenyekiti wa Kamati ya Watu Mashuhuri ya ACP Mhe Olusegun Obasanjo akiongoza kikao cha Kamati ya Watu Mashuhuri wa ACP. Kikao kinafanyika Addis Ababa Ethiopia leo. Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Dr. Leone Reyna, Mhe. Kaliate Tavola, Prof. Sebastio Izata, Prof Ibrahima Fall, Bi. Patricia Francis, Balozi Nureldin Satti, Dr Daoussa Cheriff, Mhe. Kolone Vaai, Mhe Peter Gakunu, Balozi Teshome Toga na Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala. Balozi Kamala...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiongoza kikao cha 873 cha Kamati ya Mabalozi wa ACP. Kikao hicho kimefanyika Brussels kuandaa kikao cha Baraza la Mawaziri la ACP kitanachotarajiwa kufanyika Nairobi Kenya tarehe 16-20 Juni,2014.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ABAINISHA MTAZAMO MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA AFRIKA, KARIBIANI, PASIFIKI NA JUMUIYA YA ULAYA

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akihutubia wadau wa ushirikiano kati ya nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya. Balozi Kamala alisisitiza umuhimu wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya kushirikiana katika kujenga uchumi, kukuza na kutumia teknolojia kuharakisha maendeleo na kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara yenye kunufaisha pande zote. Wadau wa ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya...

 

11 years ago

Michuzi

MHE. RAIS TEODORO NGUEMA MBASONGO AZUNGUMZA NA KAMATI YA MABALOZI WA NCHI ZA AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI (ACP)

 Mhe. Rais Teodoro Nguema Mbasongo (katikati)  wa Guinea ya Ikweta  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kamati ya Mabalozi wa ACP baada ya kuzungumza na Kamati ya Mabalozi. Mhe Rais Mbasongo amesisitiza umuhimu wa nchi za ACP kushirikiana kujenga uchumi na kufanya biashara.  Akimkaribisha Rais huyo kuzungumza na Kamati ya Mabalozi wa ACP  Balozi wa Tanzania Ubelgiji na Mwenyekiti kamati Balozi Dr. Diodorus Kamala  (wa pili kulia) amesema nchi za ACP zinapaswa kuhakikisha  Mikataba...

 

10 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WA SEKRETARIETI YA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIC AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Afrika, Karibiani na Pacific, Balozi Patrick Gomes (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania katika Jumuiya ya Ulaya, Balozi Dk. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada kumaliza kikao cha kushauriana masuala mbalimbali ofisini kwa Balozi Kamala Brussels. Kulia ni Balozi Jagne msaidizi wa Balozi Gomes.

 

11 years ago

Michuzi

kikao cha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) jijini nairobi


Mhe. Dr. Abdalah Kigoda (wa nne kutoka kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri wa nchi za ACP. Kikao hicho kimeanza leo Nairobi, Kenya. Mhe. Janet Mbene Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania Kenya Dr. Batilda Burian (wa pili kutoka kushoto) na Balozi wa Tanzania Ubelgiji (wa kwanza kulia). Mhe. Mbene yupo Kenya akihudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP).
>

 

9 years ago

Michuzi

MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI NA PACIFIKI WAMUAGA BALOZI DR. KAMALA

Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki Jumuiya ya Ulaya. Mabalozi hao wamemshukuru Balozi Kamala kwa kazi  aliyofanya ya kuongoza Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki. Balozi Kamala amemaliza kipindi chake cha kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani