Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mawakili wa Gwajima Wajibu Mapigo Waiandikia Barua Polisi Kuhusu Uhalali wa Kumtaka Gwajima Awasilishe Nyaraka 10 za Mali Zake


Mawakili wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, wameandika barua kuliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuandika kimaandishi nyaraka wanazozihitaji azipeleke pamoja na vifungu vya sheria vinavyomtaka awasilishe nyaraka hizo.Barua hiyo iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala iliwasilishwa jana mchana katika jeshi hilo, ikiwa ni siku moja baada ya jeshi hilo kumtaka Askofu Gwajima kuwasilisha nyaraka 10, Aprili 16 mwaka huu watakapoendelea na mahojiano.
Gwajima...

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Habarileo

Mawakili wa Gwajima wataka uhalali wa kupeleka nyaraka Polisi

Josephat GwajimaMAWAKILI wa Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, wameandika barua kuliomba Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuandika kimaandishi nyaraka wanazozihitaji azipeleke pamoja na vifungu vya sheria vinavyomtaka awasilishe nyaraka hizo.

 

10 years ago

Mtanzania

Mawakili wa Gwajima wamwandikia Kova barua

kovaNA AGATHA CHARLES
WAKILI wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Peter Kibatala, ameliandikia barua Jeshi la Polisi nchini akiomba vifungu vya sheria vilivyotumika kuomba nyaraka za umiliki wa vitu mbalimbali vya Askofu huyo.
Pamoja na hilo, Kibatala aliomba mteja wake huyo kuambiwa kwa maandishi juu ya vitu vinavyotakiwa kuwasilishwa kwa Jeshi hilo.
Barua hiyo ambayo Kibatala ameielekeza kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, pia nakala yake...

 

10 years ago

Mtanzania

Barua ya Gwajima yaumiza kichwa polisi

Kamishna Suleiman Kova

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova

Na Asifiwe George, Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekiri kupokea barua iliyotolewa na mawakili wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ya kulitaka kuonyesha kifungu cha sheria kinachomtaka mtu kutoa hati ya mali anazozimiliki.
Hata hivyo, jeshi hilo limekataa kuzungumzia chochote kuhusu barua hiyo, lakini limeahidi kuijibu baada ya kuwasiliana na mpelelezi wa kesi hiyo na...

 

9 years ago

Mwananchi

Gwajima kujibu mapigo ya Dk Slaa kesho Dar

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kesho anatarajia kujibu mapigo kuhusu tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye hivi karibuni alimweleza kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa viongozi wa Chadema.

 

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.
"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti...

 

10 years ago

GPL

MALI ZILIZOMZIMISHA GWAJIMA!

KWA wiki moja sasa, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba, kujisikia kizunguzungu hatimaye kuanguka na kupoteza fahamu kulikomtokea Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima wakati akihojiwa na polisi kulitokana na kuulizwa maswali yaliyohusu namna alivyozipata mali zake, Risasi Jumamosi linakupa zaidi. Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. Machi 28, mwaka huu Mchungaji Gwajima...

 

10 years ago

Mtanzania

Askofu Gwajima taabani polisi

NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

HALI ya afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana.

Askofu Gwajima alifika kituoni hapo saa 2 asubuhi akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya watano.

Katika hali ya kushangaza, wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupanda mbili, lakini alipojaribu ya...

 

10 years ago

Mtanzania

Gwajima azimia akihojiwa polisi

Asifiwe George na Humphrey Shao
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Gwajima ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Waandishi wa Mtanzania Jumamosi waliokuwa...

 

10 years ago

Mwananchi

Gwajima: Kikwete wakemee polisi

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo vya dola vinavyomfuatafuata vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa kufanya hivyo itakuwa wazi kwamba yeye ndiye anawatuma

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani