MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI KWA SASA ANAPUMULIA MASHINE MUHIMBILI
MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia...
CloudsFM
Habari Zinazoendana
11 years ago
CloudsFM29 May
YULE MTOTO ALIYEFUNGIWA KWENYE BOKSI MOROGORO HUYU HAPA AKIWA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI
Mtoto aliyekuwa amefichwa kwenye boksi mkoani Morogoro, Nasra Mvungi ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwa uchunguzi zaidi.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Morogoro, Dk Godfrey Mtei alisema Nasra alipelekwa Muhimbili juzi usiku baada ya hali yake kutoridhisha.
Alisema afya ya Nasra ilibadilika ghafla juzi asubuhi na kushindwa kupumua vizuri, jambo lililowalazimu madaktari kumpeleka Muhimbili kwa gari maalumu la wagonjwa...
11 years ago
Mwananchi23 May
Kaka wa mtoto aliyefungiwa kwenye boksi naye ‘apotea’
11 years ago
Mwananchi28 May
Mtoto aliyeishi kwenye boksi, ahamishiwa Muhimbili
11 years ago
CloudsFM29 May
HUYU NDIYE MTOTO ALIYEFUNGIWA NDANI YA BOKSI KWA MIAKA MINNE NA MAMA YAKE MLEZI ILI ASIMWAMBUKIZE VIRUSI VYA UKIMWI
Mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa), amedhulumiwa haki yake ya utu na kuteswa kwa zaidi ya miaka mitatu, kwa kufungiwa ndani ya boksi kama mnyama, ili asimuambukize mama mlezi virusi vinavyosababisha Ukimwi.
Wakizungumza na...
11 years ago
Tanzania Daima30 May
Mtoto wa boksi apumulia mashine
MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa...
11 years ago
Tanzania Daima31 May
Mtoto wa boksi aondolewa mashine
HALI ya mtoto Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne, inaendelea kuimarika baada ya kutolewa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua. Siku mbili zilizopita, Nasra aliwekewa mashine na kupata...
11 years ago
Habarileo31 May
'Mtoto wa boksi' bado apumulia mashine
MTOTO wa miaka minne aliyekuwa amefichwa kwenye boksi mkoani Morogoro, bado anaendelea kutumia mashine ya kupumua baada ya kushindwa kupumua vizuri. Hali hiyo imesababishwa na maradhi ya kichomi yanayomsumbua.
11 years ago
Habarileo28 May
'Mtoto wa boksi' yupo Muhimbili
MTOTO mwenye umri wa miaka minne aliyefungiwa ndani ya boksi kwa zaidi na miaka mitatu mkoani Morogoro, amehamishiwa katika Hos- pitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na tiba zaidi huku wataalamu wakikuna vichwa namna ya kumrudishia afya yake.
11 years ago
CloudsFM02 Jun
MTOTO ALIYEWEKWA KWENYE BOKSI KWA MIAKA MINNE KUZIKWA KWA HESHIMA ZOTE,KUAGWA KATIKA UWANJA WA JAMHURI,MOROGORO
Msiba wa mtoto Nasra Mvungi (4), aliyeteswa kwa kufungiwa katika boksi kwa miaka minne, ambako ndiko alikokuwa akipewa chakula, kwenda haja kubwa na ndogo na kulala, imeibua simanzi jijini Dar es Salaam, Morogoro na katika maeneo mbalimbali nchini.
Jana taarifa za kufariki kwa Nasra aliyekuwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, zilisambaa katika maeneo mbalimbali nchini na baadaye kuthibitishwa na Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaeshi.
Mwishoni...