Sitta: Natukanwa, ni mapambano
MWENYEKITI wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, amesema amekuwa akitishwa kupitia simu yake ya mkononi na kutaka baadhi ya vyombo vya habari na watu wanaomchukia, kutenganisha chuki hizo na Bunge Maalumu la Katiba. Akizungumza bungeni jana, Sitta alisema kwa siku anapokea ujumbe mfupi wa simu (SMS) 50 tofauti, wenye matusi jambo alilosema ni baada ya Chadema kuweka simu zake katika mtandao.
habarileo
Habari Zinazoendana
11 years ago
Habarileo27 Jun
Werema: Nina watoto halafu natukanwa?
TAFRANI iliyojitokeza bungeni juzi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema kumuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR Mageuzi) tumbili, naye kumjibu kwa kumuita mwizi imeingia katika hatua nyingine ambapo wawili hao wamekataa kusuluhishwa. Jana asubuhi baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha shughuli za Bunge, Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, aliwakuta Werema na Kafulila wakiendeleza mzozo nje ya ukumbi wa Bunge mjini...