Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


watano wachukua fomu kugombea ubunge jimbo la chalinze


Jumla ya wagombea watano wamechukua fomu za kuwania Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Bagamoyo,  Zoezi  litafungwa rasmi tarehe 12 Machi 2014 saa kumi kamili alasiri, kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Bagamoyo, David Shija.
Wagombea hao ni:-
Mathayo Torongey (CHADEMA) Phabian Skauki wa (CUF) Vuniru Hussein (NRA)  Ramadhan Mgaya (ASP)  Ridhiwani Kikwete (CCM)

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

IDD AZAN na Jumaa Mhina 'Pijei' wachukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Kinondoni na Kawe

  Mbunge wa Jimbo la Kinondoni anayemaliza muda wake, Mhe. Idd Azzan, akionesha fomu ya kuomba kuwania tena ubunge wa Jimbo la Kinondoni aliyokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Jamii UVCCM Dar es Salaam na Kamanda mstaafu wa wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni, na Wakili wa Mahakama kuu, Jumaa Mhina 'Pijei' akikabidhiwa fomu ya kuomba kuwania Ubunge Jimbo la Kawe,jana jijini Dar es Salaam kupitia...

 

9 years ago

Dewji Blog

Nyalandu achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini

FOMU

Mgombea Ubunge Jimbo la Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu akichukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kwa  MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI, Mkurugenzi Mtendaji HAJJAT MWASUMILWE.

hotubA

Nyalandu akihutubia wananchi Kinyagigi.

kinyagigi

Lazaro Nyalandu akiwa Kinyagigi.

MAPOKEZI

Wananchi wa kijiji cha Kinyagigi wakimpokea Nyalandu.

 

10 years ago

Dewji Blog

Jerry Slaa arejesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ukonga

IMG_9354

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu  aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).

Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto...

 

10 years ago

Michuzi

QS Muhonda arudisha Fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Kinondoni

 QS J Muhonda ambaye ambaye anasimamia kazi za wasanii kupitia kampuni yake ya QS leo alikua akirudisha Fomu ya Kuomba kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni.
QS amesema kuwa ameamua kuchukua fomu na kugombea nafasi hiyo ili kuleta maendeleo ya jimbo hilo na pia anauwezo na ufanisi mkubwa wa kuleta maendeleo katika jimbo hilo la Kinondoni, Lakini pia una ushawishi mkubwa kwa vijana ambao ni taifa la leo kuwafanya kuwa nguvu kazi ya Taifa hususan vijana wengi wa kinondoni ambao hawana ajira...

 

9 years ago

Vijimambo

Saada Mkuya achukua fomu za kugombea Ubunge jimbo jipya la Welezo

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alipowasili Ofisi za tume ya uchafguzi kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea Ubunge jimbo jipya la QWelezo na kuiahidi kuleta maendeleo katika jimbo hilo la WELEZO.Waziri wa Fedha , Saada mkuya akitia saini wakati wa kukabidhiwa fomu za kugombea Ubunge jimbo jipya la WelezoAfisa wa Uchaguzi akitoa maelezo kumpatia Waziri Saada Mkuya ya namna ya ujazaji wa fomu za kuwania Ubuinge

 

9 years ago

Michuzi

Anthony Mavunde achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Dodoma jijini.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma,Antony Mavunde akionesha fomu alizochukua za kugombea Ubunge katika jimbo hilo nje ya ofisi za Halmashauri ya Dodoma.  Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Antony Mavunde akipungia mamia ya mashabiki wakati akielekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Dodoma kwekuchukua fomu. Mavunde akifurahia jambo na Wafuasi wake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia chama cha Mapinduzi,Antony Mavunde akikabidhiwa fomu na Afisa...

 

10 years ago

GPL

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA‏

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto). Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William...

 

10 years ago

Michuzi

Steven Nyerere achukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kinondoni na kurudisha leo

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe, akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kinondoni, Muigizaji, Steven Mengere (kulia) katika ofisi za chama hizo eneo la Mkwajuni, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mke wa mgombea Dk. Sarah Makene. Picha na Elisa ShundaMuigizaji, Steven Mengere, akionyesha fomu ya kugombea ubunge jimbo la kinondoni kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya...

 

10 years ago

Vijimambo

KAMANDA JOHN BUYAMBA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA.

Aliekuwa Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Misungwi John Buyamba (Kulia) akionyesha fomu ya kuwania kugombea Ubunge jimbo la Ilemela.
Na:George GB PazzoMakada mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, wameendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama hicho ili kugombea nafasi za uongozi kwa ngazi za Udiwani na Ubunge.
Zaidi ya Makada sita wa chama hicho tayari wamejitokeza na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Ilemela,...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani