Ajali ya basi yaua 12 na kujeruhi 22 Iringa
Taswira kutoka eneo la ajali.
Takribani watu 12 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine 22 wakijeruhiwa baada ya basi la New Force kupata ajali leo eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na limepata ajali mchana huu.
Jitihada za kuondoa miili na kusafirisha majeruhi kuwapeleka hospitali zinaendelea.
Global Publishers
Habari Zinazoendana
9 years ago
Habarileo16 Sep
Ajali basi la Metro yaua 5, kujeruhi 39
WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 39 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Metro, kuacha njia, kutumbukia bondeni na kupinduka.
10 years ago
GPL![](http://api.ning.com:80/files/W8k9GghxLBuzok*gZsri*eUzWfAnx5jfzNu3jR57kqH7McXxnHx9*h*3mBGBE-YQGzbARFSdiiMHPjBF-c*LIpO3h2vPSi75/IMG20141216WA0003.jpg?width=650)
AJALI YA BASI YAUA SABA, NA KUJERUHI TABORA
10 years ago
GPL![](http://api.ning.com:80/files/cFSv-yJm2DTAbWDo8Za-TKdf5u7nC50pItGoaIVF0-849UFxdnQ6BRoAxlUgYS-MtUOJWMaBJzVd9phZUNZoAfre0P8xNU1E/BREAKING.gif)
AJALI YA BASI NA TRENI YAUA 5 NA KUJERUHI 24 WILAYANI KILOSA
10 years ago
Vijimambo![](http://3.bp.blogspot.com/-fac5wk09ebw/VJBkW05ZC5I/AAAAAAACUa8/qYRjxsZqpSk/s72-c/IMG-20141216-WA0046.jpg)
AJALI YA BASI LA MOHAMED TRANS YAUA WATU SITA NA KUJERUHI
![](http://3.bp.blogspot.com/-fac5wk09ebw/VJBkW05ZC5I/AAAAAAACUa8/qYRjxsZqpSk/s640/IMG-20141216-WA0046.jpg)
9 years ago
Dewji Blog02 Dec
News Alert: Ajali mbaya ya basi, yaua abiria 12 na kujeruhi vibaya 18 Singida
Pichani ni muonekana upande wa dereva wa basi la Taqbiir lenye namba za usajili T230-BRJ.
Basi la Kampuni ya Taqbiir lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Katoro-Geita, lilipofika kijiji cha Kisonzo, tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Desemba mosi mwaka huu, majira ya saa moja na nusu liligonga Tenka la Mafuta upande wa kulia wa dereva na kung’oa bati lote na kuua baadhi ya watu papo hapo na wengine walifia njiani wakipelekwa hospitali ya wilaya ya Iramba. (Picha zote na...
10 years ago
Mtanzania12 Mar
Ajali ya basi yaua 42 Iringa
WATU 42 wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mbao.
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Changalawe, Mafinga mkoani Iringa.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo aliiambia MTANZANIA kwamba basi hilo namba T438 CDE, mali ya Kampuni ya Majinjah Express lilikuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo basi hilo liligongana na lori hilo lililokuwa likitoka Iringa...
9 years ago
Mtanzania05 Jan
Ajali ya basi yaua wanne Iringa
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WATU wanne wamefariki dunia katika ajali ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Luwinzo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Ajali hiyo ilitokea jana wilayani hapa kwa kuhusisha basi hilo lenye namba za usajili T 782 ACR linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es salaam ambalo lilipata ajali asubuhi katika eneo la Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa.
Basi hilo lililokuwa likisafiri kutokea Njombe kuelekea Dar es Salaam liligongana na lori lenye namba za usajilli T 718...
11 years ago
Habarileo26 Jul
Ajali yaua 3, kujeruhi 46
WATU watatu wamekufa na wengine 46 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Uchunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
10 years ago
GPL![](http://api.ning.com:80/files/-tRXgGHTUdO0Gmm49Py-NNsCMRIYLcekNO-at-gALrqai7euc27mE19-RfjPkuFYW9Gm3yJKRZM8B1dpm6K2T-PNVHUVuJ2P/breakingnews.gif)
AJALI YAUA 16 NA KUJERUHI 75 TABORA