Ajali zaua watu 103
NA WILLIAM SHECHAMBO
WATU 103 wamefariki na 138 kujeruhiwa kwenye ajali tisa za barabarani zilizotokea hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini.
Sababu kuu iliyoelezwa kusababisha ajali hizo ni uzembe wa madereva na abiria.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed Mpinga, aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kutoa tahadhari kwa abiria kutimiza wajibu wao ikiwa pamoja na kutowatetea madereva wazembe.
Alisema kikosi hicho kimeshitushwa na ajali...
Uhuru Newspaper
Habari Zinazoendana
10 years ago
Habarileo19 Feb
Ajali za kemikali zaua watu 14
WAKALA wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), umesema mwaka jana kumetokea matukio ya ajali za kemikali 11 zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 14 na uharibifu wa tani zaidi ya 250 za kemikali.
10 years ago
Habarileo06 Sep
Ajali mbili zaua watu 47
AJALI za barabarani zimeendelea kugharimu uhai wa Watanzania, baada ya jana watu 44 kufa katika ajali mbili zilizotokea katika mikoa ya Mara na Rukwa. Kati yao, 36 wamekufa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili katika eneo la Sabasaba, wilayani Butiama katika mkoa wa Mara wakati wengine wanane wamekufa katika ajali ya lori aina ya Mitsubishi Fuso.
11 years ago
Habarileo20 Apr
Ajali zaua watu saba
WATU saba wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali za barabarani na majini wilayani Bunda Mkoa wa Mara.
11 years ago
Habarileo10 Apr
Ajali za bodaboda zaua watu 1,098
WAENDESHA pikipiki ‘bodaboda’ 870 na abiria 228 wamekufa kutokana na ajali za barabarani zilizohusisha usafiri huo katika kipindi cha mwaka jana.
11 years ago
Habarileo04 Apr
Ajali zaua watu watatu Dar
WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti ya ajali za barabarani, ikiwemo mwendesha pikipiki, Arnold Lukoga (38) aliyekufa baada ya kuangukia kichwa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,Dar es Salaam, Engelbert Kiondo alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 2:30 usiku katika Barabara ya Nyerere eneo la Tazara.
11 years ago
Habarileo09 Apr
Ajali zaua watu wanne Dar
WATU wanne wamekufa katika matukio matatu tofauti jijini Dar es Salaam ya ajali za barabarani, ikiwemo mwanafunzi wa kidato cha kwanza aliyetambuliwa kwa jina la Ally Hamadi (13) kufa baada ya kugongwa na gari akivuka barabara.
11 years ago
Tanzania Daima29 May
Ajali zaua watu milioni sita
WATU milioni sita wanakadiriwa kufa na wengine milioni 20 hadi 50 hujeruhiwa kwa ajali za barabarani kila mwaka. Takwimu hizo zimebainishwa jana na daktari bingwa wa mifupa wa Taasisi ya...
11 years ago
Mwananchi25 Jan
Ajali za bodaboda zaua watu 870
11 years ago
Habarileo21 Jan
Ajali zaua watu 26 Singida, Lindi
WATU 26 wamekufa na wengine 26 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea jana, Singida na Lindi. Ajali ya kwanza iliyoua watu 13 papo hapo na mmoja kujeruhiwa, ilitokea jana asubuhi, baada ya gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo eneo la Isuna, barabara kuu ya Singida-Dodoma.