Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Balozi Dr Kamala alipokutana na Gavana wa Hainaut nchini Ubelgiji hivi karibuni

DSCF5563

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Luxermbourg na Jumuiya ya Ulaya Dr Kamala akilakiwa na Gavana wa jimbo la Hainaut nchini Ubelgiji Bw. Tommy Luclercq hivi karibuni alipomualika katika tafrija aliyoandaa katika jimbo lake.

DSCF5691

Balozi Kamala akitia saini kitabu cha mapokezi huku gavana Tommy Luclercq akishuhudia utiaji wa saini hiyo.(picha na Maganga One).

 

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA GAVANA WA HAINAUT UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika tafrija iliyoandaliwa na Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Leclercq kuwashukuru wadau wa reli na bandari kutoka Tanzania kwa kutembelea Ubelgiji. Mhe. Leclercq ameahidi kushiriki ziara ya Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Ubelgiji watakaotembelea Tanzania mwaka huu.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Mapokezi ya Hainaut huku Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Luclercq akishuhudia....

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA NAIBU GAVANA WA KANDA YA BRABANT WALONIA YA UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi zawadi Naibu Gavana wa Kanda ya Brabant Walonia ya Ubelgiji Mhe. Isabelle Kibassa Maliba baada kufanya mazungumzo naye ofisini kwake Wavre Ubelgiji. Naibu Gavana wa Kanda ya Brabant Walonia ya Ubelgiji Mhe. Issable Kibassa Maliba akimkabidhi zawadi Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala baada kumaliza mazungumzo naye. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kutembelea kanda mbalimbali za Ubelgiji.

 

11 years ago

Michuzi

Balozi kamala akutana na balozi wa ubelgiji nchini tanzania

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ubelgiji Tanzania Mhe. Adam Koeler (wa pili kutoka kulia) baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya ziara ya wadau  wa sekta za  miundombinu ya bandari, reli na kilimo itakayofanyika Ubelgiji kuanzia tarehe 19-23 Mei, 2014. Kikao kimefanyika nyumbani kwa Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ANADI MADINI YA TANZANIA UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na  Mfanyabishara wa  Madini Bwana J. Pattyn baada ya kufanya naye mazungumzo  kuhusu  madini yanayopatikana Tanzania. Balozi Kamala amemshauri Bwana. Pattyn awahimize Wafanyabiashara wenzake washiriki katika ziara ya kibiashara itakayofanyika Tanzania mwezi Novemba, 2014 inayoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji kwa kushirikiana na taasisi ya AWEX ya Ubelgiji.

 

10 years ago

Vijimambo

BALOZI SEIF AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN NA BALOZI MALAWI NCHINI TANZANIA, PIA AZUNGUMZA NA GAVANA MKUU WA JIMBO LA SIUSTAN NA BALACHESTAN

Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan Balozi Batilda Buriani akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika kuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania Bibi Hawa Ndolowe aliyefika Ofisini kwake kujitambulisha rasmi.
Balozi Seif akisalimiana na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KAMPUNI YA TRACTEBEL ENGINEERING S.A. YA UBELGIJI

 Balozi wa Tanzania  Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya  ya Ulaya Dr. Diodorus  Kamala akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi pamoja na wadau kutoka Tanzania katika sekta mbalimbali za usafirishaji wa majini ,anga na reli.Kulia kwa Dr Kamala ni Mkurugenzi wa Tractebel Engineering nchini Ubelgiji bwana Hein Dirix na kushoto kwa Balozi Kamala ni Mh. Nazir Karamagi mkurugenzi mtendaji wa Tanzania International Container Terminal Service Limited. Picha na Maganga One

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MEYA WA MANISPAA YA COVVIN UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) amekutana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Covvin ya Ubelgiji Bwana Raymond Douniaux (kulia). Balozi Kamala amemuomba Mhe Meya huyo kutangaza Utalii wa Tanzania na amemkabidhi vifaa ya kutangaza utalii wa Tanzania.

 

11 years ago

GPL

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KAMPUNI YA TRACTEBEL ENGINEERING S.A. YA UBELGIJI‏

Balozi wa Tanzania  Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya  ya Ulaya Dr. Diodorus  Kamala akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi pamoja na wadau kutoka Tanzania katika sekta mbalimbali za usafirishaji wa majini ,anga na reli.Kulia kwa Dr Kamala ni Mkurugenzi wa Tractebel Engineering nchini Ubelgiji bwana Hein Dirix na kushoto kwa Balozi Kamala ni Mh:Nazir Karamagi mkurugenzi mtendaji wa Tanzania International Container...

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KIWANDA CHA KAMPUNI YA ABC UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji,Dk. Diodorus Kamala akiangalia mtambo wa kufua umeme unaotengenezwa na kiwanda cha ABC cha Ubelgiji. Mtambo huo ni kati ya mitambo itakayopelekwa Mpanda Tanzania.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani