Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


BALOZI MWAPACHU ARUDISHA RASMI KADI YA CCM

Balozi Mwapachu (kulia) akikabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba. KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu leo amerejesha kadi yake ya uanachama ofisi za chama hicho zilizopo Mikocheni A jijini Dar es Salaam. Balozi Mwapachu aliyetangaza kukihama chama hicho juzi (Jumanne) kwa madai...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Mwananchi

Balozi Mwapachu arudisha kadi atangaza kujiunga Ukawa

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu leo amerudisha kadi ya uanachama katika ofisi za CCM Kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

 

9 years ago

Mtanzania

Mwapachu arudisha kadi ya CCM, Tanu

IMG_9794NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu, amerejesha rasmi kadi za Chama cha Tanu na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kadi hizo alizirudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Mikocheni A jijini Dar es Salaam jana na kuzikabidhi kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Kata ya Mikocheni, Sudi Odemba.

Mwapachu ambaye ni kada mkongwe wa chama hicho, alisema kadi ya Tanu yenye namba 819820 aliipata Aprili 6,...

 

9 years ago

Vijimambo

BALOZI JUMA MWAPACHU KUJIVUA RASMI UANACHAMA CCM KESHO

NAJIVUA UANACHAMA WA CCMNdugu zangu,
Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU Youth League. Nimepata fursa ya kuwa kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia kesho mimi si mwanachama wa CCM tena. Natoa...

 

9 years ago

Mzalendo Zanzibar

TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU. NAJIVUA UANACHAMA WA CCM

Juma Mwapachu Ndugu zangu, Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha […]

The post TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU. NAJIVUA UANACHAMA WA CCM appeared first on Mzalendo.net.

 

9 years ago

Mwananchi

Balozi Juma Mwapachu ajitoa uanachama CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Juma Mwapachu leo ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho kutokana na chama kupoteza dira.

 

9 years ago

Mwananchi

Balozi Mahiga akabidhiwa mikoba ya Balozi Mwapachu

Balozi Augustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kuziba nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Balozi Juma Mwapachu.     

 

5 years ago

Michuzi

SUMAYE AKABIDHIWA RASMI KADI YA CCM NA DK BASHIRU, AGOMA KUFUNGUKA KILICHOMUONDOA AWALI


Charles James, Globu ya Jamii

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekabidhiwa rasmi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo hii jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally.

Sumaye amekabidhiwa kadi hiyo leo baada ya kutangaza kurejea CCM Februari 10 mwaka huu akitokea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile alichoeleza kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho kikuu cha upinzani.

Akizungumza wakati akimkabidhi kadi, Dk Bashiru amesema kurejea kwa Sumaye ni faida...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi Seif akabidhi kadi kwa wanachama wapya 15 wa CCM Mkoa wa Magharibi,Zanzibar

Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM Shina nambari 23 la Tawi la CCM Fuoni Bibi Faiza Chande Ameir.Kushoto ya Balozi ni Mwenyekiti wa Shina Nambari 23 la Tawi la CCM Fuoni Nd. Daudi Khamis, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf na Katibu wa CCM Mkoa huo Aziza Ramadhan Mapuri. Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Mwanakwerekwe Ndugu Khamis Juma Msonge akimkaguza Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa...

 

10 years ago

Michuzi

LOWASSA AJIUNGA RASMI NA UKAWA,AKABIDHIWA KADI RASMI YA UANACHAMA CHADEMA.

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo. Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) . Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani