Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


balozi Seif Ali Iddi atembelea msitu wa Muyuni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Maliasili Dr. Bakar Ased akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar umuhimu wa eneo ya hifadhi ya Misitu la Muyuni kwa ustawi  bora ya maisha ya wananchi wa ukanda wa Kusini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akitembelea msitu wa hifadhi Muyuni kuangalia maeneo ambayo baadhi ya watu wameamua kulima kilimo chengine mchanganyiko. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Kilimo na Maliasili Mh. Sira Ubwa Mwamboya na...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi atembelea Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B”

Na Othman Khamis AmeSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haipendelei kuona Wananchi katika baadhi ya shehia wanalumbana na kufikia hatua ya kuhitilafiana katika mambo ambayo wakiamua kukaa pamoja katika kuyajadili kwa njia ya vikao yanaweza kurekebishika bila ya kutumika nguvu za Serikali Kuu. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wazee na Viongozi wa Shehia za Muyuni “A “ na Muyuni “B” katika kikao cha kujadili matatizo yaliyojitokeza...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi atembelea Kisiwa cha panza, Mkoa wa Kusini Pemba.

Na Othman Khamis Ame, OMPR  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Hakmashauri Kuu ya Taifa ya  CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Chama cha Mapinduzi kina wajibu wa kuhakikisha kinashinda kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 ili kiendelee kusimamia uhimili wa amani ya Taifa iliyopo hivi sasa. Balozi Seif alisema hayo wakati akizungumza na Viongozi pamojana Wana CCM wa Kisiwa Panza Wilaya ya Makoani Pemba mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi la Mtondooni Kisiwani...

 

10 years ago

Michuzi

Balozi seif ali iddi azindua maskani kijijini kinazini, Mtambwe Kusini

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Chama hicho kiko makini katika kumuengua Mwanachama wake ye yote anayetumia hila katika mchakato wa kutaka achaguliwe kuwa Kiongozi kupitia chama hicho. Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na Vijana walioamua kutoka chama cha Upinzani na kujiunga na CCM ambapo wameanzisha Maskani iliyopewa jina la Balozi Seif Maskani hapo katika Kijiji cha Kinazini Mtambwe Kusini. Balozi Seif ambae alipata wasaa wa...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi atembeela Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni Shehia ya Kidoti Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhusiana na masuala ya huduma za maji na umeme.Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji, kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi seif ali iddi afunguwa Kituo cha Afya Cha Pwani Mchangani Wilaya ya Kaskazini “A”, Unguja

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa sambamba na Mwakilishi wa Hoteli ya Waride Resort  Bwana Massliano  Bramucci wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Huduma za akina Mama wajawazito katika Kijiji cha Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.  Mfadhili wa ujenzi wa Kituo cha akina mama wajawazito cha Pwani Mchangani Bwana Massiliano Bramucci akitoa maelezo kwa  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara tu baada ya kukifungua Kituo hicho.   Balozi...

 

9 years ago

Michuzi

BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA MRADI WA MAJI NA SALAMA KASKAZINI UNGUJA

 Balozi Seif Ali Iddi akizindua Mradi wa Maji safi na salama katika kisiwa cha Tumbatu ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Balozi Seif akimtwisha ndoo ya Maji Bibi Miza Ali Haji mara baada ya kuuzindua mradi wa maji safi na salama katika kisiwa cha Tumbatu kiliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu waliohudhuria uzinduzi wa maji safi na...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi seif ali Iddi atembelea Kijiji cha Kilombero

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Nd. Hassan Ali Hassan alisema shirika lake linakusudia kutumia rasilmali ilizonazo katika kuhakikisha huduma za umeme zinapatikana kwenye kisima cha maji cha Kijiji cha Kilombero ili kuwaondoshea usumbufu wa huduma za maji safi  kwa Wananchi wa Kijiji hicho. Alisema kazi hiyo itakayoanza wakati wowote kuanzia sasa inatarajiwa kukamilika sambamba na ulazwaji wa mabomba ya maji utakaofanya na wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA }...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi atembelea Mabanda ya Maonyesho ya miaka 50 ya muungano

Licha ya baadhi ya wabunge wa Upinzani wa Bunge Maalum la Katiba kuamua kususia kuendelea kushiriki katika mjadala wa Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa ndani ya Bunge hilo Kundi kubwa la Wajumbe hao waliobaki wataendelea kuchapa kazi waliyotumwa na Wananchi bila ya kujali uwamuzi uliochukuliwa na wale walioamua kutoka nje ya mjadala huo.  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mbunge wa Bunge hilo Maalum la Katiba Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya...

 

11 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi asaidia vifaa vya ujenzi kwa Ofisi ya CCM Tawi la Kazole, Kaskazini Unguja

Othman Khamis Ame, OMPR Zaidi ya asilimia 95% imefikiwa katika ujenzi wa Matawi ya Kisasa ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Jimbo la Kitope liliomo katika Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja.  Hali hiyo imekuja kufuatia hatua za ukamilishaji wa Linta katika Tawi la Chama cha Mapinduzi la Kazole likiwa miongoni mwa Matawi 19 ya Kisasa yaliyo kwishajengwa kati ya Matawi 20 yaliyomo ndani ya Jimbo hilo.  Katika kuunga mkono harakati za Wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani