Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Chadema yaibwaga polisi kesi ya marehemu Mawazo

Picha ya Mawazo (2)NA BENJAMIN MASESE, MWANZA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza, imetupa zuio la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, RPC Charles Mkumbo kuzuia kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), marehemu Alphonce Mawazo.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji Lameck Mlacha na kuwapa ruksa ndugu na viongozi wa chama hicho kutoa heshima za mwisho sehemu yoyote itakayofaa, huku akisema amri ya kamanda huyo wa Mwanza ni batili kisheria.

Katika hukumu hiyo, mahakama ilisema...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Mtanzania

Kesi ya marehemu Mawazo yatinga kortini

MboweNA BENJAMIN MASESE, MWANZA

HATIMAYE Charles Lugiko ambaye ni baba mdogo wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa  Geita, marehemu Alphonce Mawazo, amefungua kesi ya kupinga uamuzi wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mwanza, kuwazuia kuaga mwili wa mtoto wao.

Kesi hiyo ilifunguliwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ambapo wanasheria watatu wa Chadema walijitokeza kwa ajili ya kumtetea.

Jeshi hilo, lilizuia mwili wa marehemu Mawazo usiagwe jijini Mwanza...

 

9 years ago

StarTV

Chadema yafungua kesi ya madai  kuhusu Zuio La Kuaga Mwili Wa Mawazo

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefungua kesi ya madai katika mahakama kuu kanda ya Mwanza kutengua zuio la jeshi la polisi mkoani humo kuzuia wafuasi wa chama hicho wasiuage mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Geita.

Kesi hiyo namba 10 ya mwaka 2015 imefunguliwa kwa hati ya dharura sana kwa niaba ya mlalamikaji mchungaji Charles Lugiko ambaye ni baba mlezi wa marehemu.

Katika mahakama kuu kanda ya Mwanza wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema...

 

10 years ago

Mwananchi

Chadema yaibwaga CCM mahakamani

>Chama cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imezidi kupata pigo baada ya Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji 16 vya mji mdogo wa Mirerani, kwa maelezo kuwa ulikiuka sheria na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

 

10 years ago

Michuzi

KESI WAFUASI WA CHADEMA KUVAMIA POLISI YASOMWA LEO MAHAKAMANI

UPANDE wa Jamhuri katika kesi inayowakabili wafuasi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umedai mahakamani kwamba washtakiwa hao walikiuka amri halali ya Jeshi la Polisi baada ya kuvuka kizuizi kilichowekwa eneo la Makao Makuu ya  jeshi hilo.
Kadhalika, washtakiwa hao Ngaiza Kamugisha (28)  dereva, mkazi wa Vingunguti, Benito Mwapinga (30) Fundi nguo mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally na Eliasante Bugeji (51) Mhasibu wa CCBRT mkazi wa Komakoma Kinondoni, Dar es Salaam, wanadaiwa...

 

9 years ago

Mtanzania

Kesi ya Mawazo kutolewa hukumu leo

Alphonce  MawazoNA BENJAMIN MASESE, MWANZA

JAJI wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Lameck Mlacha, anatarajia kutoa hukumu juu ya mvutano wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Geita marehemu Alphonce Mawazo jijini Mwanza.

Jaji Mlacha anatarajia kutoa hukumu hiyo leo saa saba mchana baada ya pande zote mbili kueleza hoja zao.

Mawakili wa Serikali, Seth Mkemwa na Emilly Kilia ambao wanamtetea Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo aliyezuia...

 

9 years ago

Michuzi

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA KESHO NA MAHAKAMA


Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa taarifa kwa wananchi baada ya Chadema Kufungua Kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga kuzuiliwa kwa mwili wa Marehemu Mawazo kuagwa Jijini Mwanza.
Na George Binagi - GB Pazzo wa Binagi Media Group
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na...

 

9 years ago

Mwananchi

Mahakama yatupa pingamizi la Serikali kesi ya Mawazo

Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza jana ilitupa pingamizi la Serikali la kuitaka itupilie mbali kesi ya kutaka kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo na hivyo kutoa fursa kwa familia ya marehemu kufungua kesi ya msingi.     

 

9 years ago

Michuzi

KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA KUHUSU HATMA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO

Jana Novemba 26,2015 Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitengua zuio la Jeshi la Polisi Mkoani hapa la kuzuia ibada ya mazishi ya kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Geita Alphonce Mawazo alieuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu Mkoani humo.
BONYEZA PLAY KUSIKILIZA  

 

9 years ago

StarTV

Mahakama kuu Mwanza yaahirisha kesi Kuaga Mwili Wa Alphonce Mawazo

Mahakama kuu Kanda ya Mwanza imeahirisha kesi iliyofunguliwa na familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo kupinga amri ya Polisi kuzuia mwili wake usiagwe jijini Mwanza.

Kesi hiyo namba 11 ya mwaka 2015 ambayo imefunguliwa mchana wa leo ikisimamiwa na wakili James Milya na John Malya kutoka Chadema na itatajwa tena Novemba 25 mwaka huu

Mapema asubuhi mahakama kuu kanda ya Mwanza imeruhusu maombi ya baba mdogo wa...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani