Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


JUST IN: mnenguaji aisha madinda afariki dunia leo

ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia leonyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam. Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika. Akizunumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.“Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Bongo Movies

TANZIA:Aliyekuwa mnenguaji wa muziki wa Bendi, Aisha Madinda Afariki Dunia Hii Leo

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar

Aisha madinda ambae jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika  Hospitali ya Ocean Road jijini Dar na alipata umaarufu mkuwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye  Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasinia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu akiwana watu...

 

10 years ago

Mwananchi

Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia

Aliyekuwa mnenguaji mahiri wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Madinda amefariki dunia leo katika Hospitali ya Mwananyamala, jiji Dar es Salaam.

 

10 years ago

Bongo Movies

TANZIA:Aliekuwa mneguaji wa muziki wa Bendi Aisha Madinda Afariki Dunia Hii Leo

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar

Aisha madinda ambae jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika  Hospitali ya Ocean Road jijini Dar na alipata umaarufu mkuwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye  Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’.

Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasinia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu akiwana watu...

 

10 years ago

GPL

AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.…

 

10 years ago

Mwananchi

Pumzika kwa amani mnenguaji Aisha Madinda

Jumatano hii iliyopita, mmoja kati ya wanenguaji waliokuwa nguzo ya Bendi ya The African Stars Band, hasa katika safu ya unenguaji, Aisha Mohamed Mbegu `Madinda’ alifariki dunia.

 

10 years ago

CloudsFM

AISHA MADINDA KUZIKWA LEO

Aliyekuwa mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta na Extra Bongo,marehemu Aisha Madinda anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Kigamboni,jijini Dar.

Hapa Aisha akiwa na watoto wake enzi ya uhai wake.

Kwa mujibu wa mtoto wake wa kwanza aitwaye Faisal Madinda alisema kuwa asubuhi wako katika hospitali ya Mwananyamala kuuandaa mwili wa marehemu na baadaye wataupeleka nyumbani kwao maeneo ya Kigamboni na atazikwa leo saa kumi jioni.

 

 

10 years ago

Michuzi

AISHA MADINDA AZIKWA LEO KIBADA,KIGAMBONI

WAKURUGENZI wa bendi hasimu za dansi Tanzania, African Stars, Asha Baraka na Extra Bongo, Ali Choki, leo wameongoza mamia ya waombolezaji kumzika aliyekuwa mnenguaji wa zamani wa bendi hizo, Aisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Mazishi ya Aisha Madinda yamefanyika leo kwenye Makaburi ya Kijiji cha Mikwambe, Kigamboni jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kufanyika jana kutokana na zuio la Jeshi la Polisi, kupisha uchunguzi wa sababu za kifo cha ghafla cha mnenguaji huyo.
Baada ya uchunguzi...

 

10 years ago

CloudsFM

HATIMAYE MWILI WA AISHA MADINDA WAFANYIWA UCHUNGUZI KUZIKWA LEO MCHANA

Baada ya danadana nyingi, hatimaye mwili wa mnenguaji Aisha Madinda unafanyiwa upasuaji muda huu katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao Saluti5, mkurugenzi wa Aset Asha Baraka amebainisha kuwa upasuaji umeanza dakika 10 zilizopita na ni zoezi linalotarajiwa kuchukua masaa mawili.

Asha Baraka amesema baada ya zoezi hilo, watauosha mwili wa marehemu katika msikiti ulioko hapo Muhimbili ikiwa ni pamoja na uvishaji wa sanda kabla ya kuelekea nyumbani kwao...

 

10 years ago

CloudsFM

Lala salama Aisha Madinda

Jeneza likiwa tayari kusubiri mwili wa marehemu Aisha Madinda msibani maeneo ya Kigamboni,jijini Dar.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani