Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Maafa Shinyanga *Barafu yafunika kijiji, watu 42 wafariki dunia *Zaidi ya 91 wajeruhiwa, mamia wasombwa na maji *Nyumba zabomolewa, mifugo mingi nayo yafa

IMG-20150304-WA0018Paul Kayanda na Kadama Malunde, Kahama

WATU 42 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 91 wamejeruhiwa vibaya baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kijiji cha Mwakata, Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Pamoja na vifo hivyo, nyumba za makazi na majengo ya taasisi mbalimbali, yamebomolewa na mafuriko yaliyosababishwa mawe kusambaa kijiji kizima.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, aliiambia MTANZANIA kwa simu jana kwamba zaidi ya kaya 100...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Dewji Blog

Breaking News: Watu 10 wafariki dunia katika ajali ya basi Shinyanga na 51 wajeruhiwa

vpo

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi, Justus Kamugisha.

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha Modewji blog ni kuwa bado jeshi la Polisi na wasamaria wema wanaendelea kuokoa majeruhi na maiti wa ajali ya gari iliyotokea muda wa masaa mawili yaliyopita kwa kuuhusisha basi la Unique namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye...

 

10 years ago

Vijimambo

WATU 10 WAFARIKI NA WENGINE ZAIDI YA 40 WAJERUHIWA KWENYE AJALI YA BASI LA UNIQUE NA LORI MKOANI SHINYANGA

 Winchi likinyanyua basi baada ya ajali ambapo watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa kutokana na ajali ya basi la Unique na lori kugongana uso kwa uso  mkoani Shinyanga leo. Zoezi la kunyanyua mabaki ya basi hilo likiendeleaWinchi likiwa kazini huku wanahabari wkirekodi tukio la kunyanyuliwa basi hilo.

CHANZO: MICHUZI BLOG

 

10 years ago

CloudsFM

Haya ndiyo mabonge ya barafu(mawe) yaliyoua watu zaidi ya 42 Kahama,Shinyanga

Haya ndiyo mabonge ya barafu(mawe) yaliyoua watu zaidi ya 42 na wengine 91 kujeruhiwa baada ya kuamkia jana katika kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

WATU 42 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 91 wamejeruhiwa vibaya baada ya mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha katika Kijiji cha Mwakata, Kata ya Isaka, Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga. Pamoja na vifo hivyo, nyumba za makazi na majengo ya taasisi mbalimbali, yamebomolewa na mafuriko yaliyosababishwa mawe...

 

9 years ago

Michuzi

WATU SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUUNGUA NA MOTO NA WENGINE KUMI WAJERUHIWA

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma Ferdnand Mtui  akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ajali ya moto iliyotokea Mkoani Kigoma. Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma. Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya matibabu katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma.
                                               Na Editha Karlo wa blog wa jamii,Kigoma
WATU saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali...

 

5 years ago

Michuzi

BREAKING NEWZZZZZ: WATU 18 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 15 WAJERUHIWA KWA AJALI WILAYANI MKURANGA.


Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kamanda Lyanga amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Aprili 15, 2020 na kwamba imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amebainisha...

 

9 years ago

Global Publishers

Watu 8 akiwemo Msaidizi wa IGP Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Dodoma

Polisi Eneo la tukio, maaskari wakiukagua mwili wa marehemu.polisiii 1Gari walilopata nalo ajali

WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa  familia moja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Amesema baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi...

 

10 years ago

Vijimambo

WATU ZAIDI YA 2,000 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI NEPAL

 Siku moja baada ya kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi, Nepal imeshuhudia tetemeko lingine kubwa lililoelezewa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kathmandu.  Maofisa nchini humo wamesema kuwa vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi ya kuwatafuta watu walionusurika, na wanahofu kuwa idadi ya watu waliofariki dunia inaweza kuongezeka.Wananchi wakiwa wamekusanyika katika maeneo ya wazi mitaani mjini Kathmandu baada ya kutokea kwa tetemeko hilo. Tetemeko hilo...

 

11 years ago

Mwananchi

Tisa wafariki dunia, 10 wajeruhiwa

Watu tisa wamekufa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugonga lori la mizigo aina ya Fiat, Iveco, lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa Barabara ya Mwanza - Musoma.

 

11 years ago

Mwananchi

Watu 11 wafariki ajali ya basi, 55 wajeruhiwa

Abiria 11 waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Burudani kutoka Korogwe kuelekea Dar es Salaam akiwamo dereva wamefariki, huku wengine 55 wakijeruhiwa baada ya basi hilo aina ya Nissan kuacha njia na kupinduka kwenye kona wakati likijaribu kupishana na lori aina ya Fuso.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani