Magufuli – Nitapasua majipu
Agatha Charles na Aziza Masoud
RAIS John Magufuli jana alilizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano kwa kurejea mambo aliyoyaahidi wakati wa kampeni zake za urais huku akijipa jukumu jipya aliloliita la kupasua majipu.
Katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge hilo iliyochukua muda wa masaa mawili, Rais Magufuli alisisitiza kuwa amejipa kazi ya kupasua majipu yanayoitesa serikali ili kuijenga upya Tanzania na kurejesha matumaini yaliyopotea ya Watanzania.
Hotuba hiyo ambayo ni ya kwanza...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania08 Dec
Magufuli atumbua Majipu 23
*Atengua uteuzi wa katibu Mkuu Uchukuzi, bosi Bandari
*Vigogo TPA wasimamishwa kazi, wawekwa chini ya ulinzi
Na Fredy Azzah, Dar es Salaam
MPANGO wa Rais Dk. John Magufuli wa kutumbua majipu, safari hii umegeuka na kung’oa vigogo 23 wa Mamkala ya Bandari (TPA) pamoja na kuvunja Bodi ya Wakurugenzi ya mamlaka hiyo.
Bodi hiyo ilikuwa na vigogo kadhaa akiwamo Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson na Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Udhibiti ya Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu.
Hatua ya...
9 years ago
Habarileo08 Dec
Magufuli aendelea kutumbua majipu
RAIS John Magufuli ameendelea kutumbua majipu katika maeneo mbalimbali yenye harufu ya ufisadi, ambapo safari hii ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya kupisha uchunguzi dhidi ya matumizi mabaya ya kiasi cha Sh bilioni 13 katika Shirika la Reli Tanzania (TRL).
9 years ago
Mwananchi28 Nov
Majipu matano sugu kwa Dk Magufuli
9 years ago
Dewji Blog28 Dec
Kanisa la Pentekoste Singida lamuombea Rais Magufuli nguvu ya kuendelea kutumbua majipu nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Na Nathaniel Limu, Singida
KANISA la Pentekoste (FPCT) Tanzania la mjini kati Singida limetumia maadhimisho ya siku ya kuzaliwa (krismasi) kwa Yesu Kristo, kumwombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mungu aendelee kumpa afya,nguvu na ujasiri wa kutumbua majipu.
Maombi hayo maalum,yalifanywa na waumini wa kanisa hilo wakiongozwa na mchungaji Philipo Sospeter,kwa kile kilichodaiwa kuwa Rais Magufuli ameanza vizuri kuwatumikia...
9 years ago
Dewji Blog26 Dec
Waziri Nape Nnauye awataka Watanzania kuendelea kumuombea Rais Dk John Pombe Magufuli, kazi ya kutumbua majipu ni ngumu na ina vikwazo vingi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali...
9 years ago
Habarileo26 Dec
Utumbuaji majipu wazaa matunda
HATUA anazozichukua Rais John Magufuli, katika kukabiliana na ufisadi ndani ya taasisi na idara za Serikali, zimeanza kuzaa matunda. Hatua hizo ambazo zinafahamika kama ‘kutumbua majipu’, pia zimeonesha kuungwa mkono na wasomi, wananchi, washirika wa maendeleo na mataifa mbalimbali ya nje.
9 years ago
Mtanzania06 Jan
Mawaziri wazidi kutumbua majipu
NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KASI ya utendaji kazi wa mawaziri wa Rais Dk. John Magufuli, imezidi kukolea baada ya mawaziri wawili kwa nyakati tofauti kuwasimamisha kazi vigogo walio chini yao kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Uamuzi wa kwanza umechukuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ambaye jana alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Mohamed Kilongo kwa kushindwa kutimiza wajibu...
9 years ago
Mtanzania19 Dec
Yanga yatamba kutumbua majipu
NA ADAM MKWEPU
UONGOZI wa Yanga umetamba kuendelea kutumbua majipu katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuhakikisha wanashinda michezo yake mbalimbali ya ligi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, alisema kuwa wamejiandaa kupata ushindi dhidi ya Stand United katika mchezo wao utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, licha ya ‘figisufigisu’ wanazoendelea kufanyiwa na wapinzani wao.
“Tutaendelea kutumbua majipu, licha ya...
9 years ago
Habarileo07 Jan
Mawaziri wacharuka kutumbua majipu
MAWAZIRI wa Serikali ya Awamu ya Tano wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wameendelea kuzuru maeneo mbalimbali nchini wakitoa matamko mazito sanjari na kuendelea ‘kutumbua majipu’ .