Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mahakama ya Kadhi, ripoti ya Msolla kutikisa Bunge

Spika wa Bunge, Anna Makinda.BUNGE linaendelea na mkutano wake wa 18, ambao kamati mbalimbali zitaendelea kuwasilisha taarifa kwa ajili ya majadiliano. Licha ya kamati za kisekta na zisizo za kisekta, kabla ya Bunge kuahirishwa wiki hii, pia Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekezaji kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi, pia itawasilisha taarifa yake.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mtanzania

Mjadala Mahakama ya Kadhi wazidi kutikisa Bunge

Bunge

Bunge

NA WAANDISHI WETU, DODOMA

MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, Abdallah Mtutura (CCM), amewataka wajumbe wa Bunge hilo ambao ni Waislamu, washirikiane kuipinga Rasimu ya Katiba kama Mahakama ya Kadhi haitaruhusiwa katika Katiba mpya.

Akichangia sura za nne na 10 za Rasimu ya Katiba bungeni mjini hapa juzi, Mtutura alisema kitendo cha baadhi ya wajumbe kuonyesha dalili za kuipinga mahakama hiyo, hakiwezi kukubalika kwa kuwa ni muhimu kwa Waislamu wanaoiamini.

“Mheshimiwa Makamu...

 

10 years ago

Mwananchi

Wabunge wawe wamoja mijadala kuhusu Ripoti ya CAG, Mahakama ya Kadhi

Bunge jana lilianza mkutano wake wa 18 mjini Dodoma likiwa na masuala mengi mazito katika ajenda yanayopaswa kujadiliwa katika muda mfupi tu wa wiki mbili. Hicho ni kikao chake cha kwanza mwaka huu, ambacho kinakuja baada ya mkutano wake wa 16/17 uliofanyika Novemba mwaka jana na kugubikwa na mjadala mkali kuhusu uchotwaji wa fedha kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow. Baadhi ya watendaji serikalini wamefikishwa mahakamani, huku mawaziri wawili na mwanasheria mkuu wa Serikali wakijiuzulu.

 

10 years ago

Mtanzania

Mahakama ya Kadhi yazikwa

Samia Hassan Suluhu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan

Rachel Mrisho, Dodoma

SUALA la Mahakama ya Kadhi ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba na kuundiwa kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, limezikwa rasmi.

Hali hiyo imejidhihirisha jana kutokana na kutozungumziwa katika uwasilishaji wa maoni ya walio wengi, wakati kamati hizo zikiwasilisha maoni yake juu ya sura ya tisa na 10.

Imedaiwa...

 

10 years ago

Mwananchi

Mahakama ya Kadhi Utata

Wajumbe wa kamati tatu za Kudumu za Bunge ambazo wenyeviti wake wanatakiwa kuvuliwa nyadhifa zao kutokana na kuhusika katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow, ‘wanasuasua’ kuwaondoa na kuchagua viongozi wengine.

 

10 years ago

Habarileo

Mahakama ya Kadhi yawekwa kiporo

SUALA la Mahakama ya Kadhi limeleta mjadala mkali katika majadiliano na wabunge wameamua suala hilo lisiingizwe kwenye Katiba. Mjadala huo mkali uliibuka katika Kamati namba Saba ilipojadili sura ya Nne ya kwenye rasimu hiyo inayozungumzia juu ya uhuru wa imani ya dini ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Ngwilizi alisema baada ya mjadala mkali wamekubaliana kutoingizwa kwenye Katiba.

 

10 years ago

Habarileo

Mahakama ya Kadhi yasogezwa mbele

Mizengo PindaWAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameeleza sababu za Bunge kushindwa kujadili miswada kadhaa, ikiwemo uliohusu Marekebisho ya Sheria ya Kiislamu, inayotambua Mahakama ya Kadhi.

 

10 years ago

Habarileo

Mahakama ya Kadhi yawagawa wabunge

MAHAKAMA ya Kadhi imetikisa mjadala wa Bunge Maalumu la Katiba jana. Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya wajumbe ambao walipata fursa ya kuchangia waliendelea kuwashawishi wenzao wakubali mahakama hiyo iingizwe kwenye Katiba kwani ni chombo muhimu kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

 

10 years ago

Habarileo

JK aweka msimamo Mahakama ya Kadhi

Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Freddy Maro).RAIS Jakaya Kikwete amefafanua msimamo wa Serikali katika mjadala unaoendelea wa Mahakama ya Kadhi, na kuweka wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuianzisha, wala kuiendesha.

 

10 years ago

Mwananchi

Pinda aiokoa Mahakama ya Kadhi

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alilazimika kuokoa jahazi la ‘kuzama’ kwa Katiba Mpya kwa kupoza hasira za Waislamu kuhusu Mahakama ya Kadhi kutoingizwa kwenye Katiba inayopendekezwa.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani