JK aweka msimamo Mahakama ya Kadhi
RAIS Jakaya Kikwete amefafanua msimamo wa Serikali katika mjadala unaoendelea wa Mahakama ya Kadhi, na kuweka wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuianzisha, wala kuiendesha.
habarileo
Habari Zinazoendana
10 years ago
Uhuru Newspaper
Kardinali Pengo aweka msimamo
Aonya matukio ya ugaidi si mambo ya dini Awataka wanaoamini wasambaze ujumbe
NA MWANDISHI WETU
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, amesema msimamo wake kuhusu katiba inayopendekezwa, uko pale pale na ametaka wanaoamini alichosema, wasambaze ujumbe wake kwa wengine.

11 years ago
Uhuru Newspaper
Dk. Sheni aweka msimamo bei ya karafuu
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kutekeleza uamuzi wake wa kuwapatia wakulima bei ya karafuu ya asilimia 80 ya bei ya soko la nje.
Dk. Sheni alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wakulima wa zao hilo wakati akizindua rasmi msimu wa ununuzi wa karafuu wa mwaka 2014/2015 uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba.

Alibainisha kuwa huo ni uamuzi wa kisera na...
11 years ago
Mwananchi05 Mar
Kardinali Pengo aweka wazi msimamo wa Kanisa
11 years ago
Habarileo20 Sep
Katibu mpya wa CCM Arusha aweka msimamo
KATIBU mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Alphonce Kinamhala ameingia ofisini kuanza kwa kazi kwa kukataa majungu.
11 years ago
Mtanzania05 Sep
Mahakama ya Kadhi yazikwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan
Rachel Mrisho, Dodoma
SUALA la Mahakama ya Kadhi ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba na kuundiwa kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, limezikwa rasmi.
Hali hiyo imejidhihirisha jana kutokana na kutozungumziwa katika uwasilishaji wa maoni ya walio wengi, wakati kamati hizo zikiwasilisha maoni yake juu ya sura ya tisa na 10.
Imedaiwa...
10 years ago
Mwananchi19 Jan
Mahakama ya Kadhi Utata
10 years ago
Mtanzania27 Jan
Maaskofu:Mahakama ya Kadhi ya Kibaguzi
JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF) limepinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, likiitaka Serikali iuondoe bungeni kwa madai kuwa ni wa kibaguzi na upo kinyume na matakwa ya Katiba.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014, unapendekeza pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ya mwaka 1964.
Maaskofu na wajumbe wa jukwaa hilo walikutana Januari 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushauri Serikali iondoe muswada huo bungeni...
10 years ago
Mtanzania30 Mar
Mahakama ya Kadhi yawavuruga wabunge
Na Debora Sanja na Fredy Azzah, Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana nusura wazichape kavukavu baada ya kutofautiana juu ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wabunge hao wakiwa katika semina iliyohusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali, ambapo miongoni mwa sheria zilizomo ndani yake ni pamoja na ile ya Mahakama ya Kadhi.
Sakati hilo lilitokea katika semina kuhusu muswada huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni keshokutwa...
10 years ago
Habarileo08 Feb
Mahakama ya Kadhi yasogezwa mbele
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameeleza sababu za Bunge kushindwa kujadili miswada kadhaa, ikiwemo uliohusu Marekebisho ya Sheria ya Kiislamu, inayotambua Mahakama ya Kadhi.