Maaskofu:Mahakama ya Kadhi ya Kibaguzi
JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF) limepinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, likiitaka Serikali iuondoe bungeni kwa madai kuwa ni wa kibaguzi na upo kinyume na matakwa ya Katiba.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014, unapendekeza pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ya mwaka 1964.
Maaskofu na wajumbe wa jukwaa hilo walikutana Januari 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushauri Serikali iondoe muswada huo bungeni...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mtanzania29 Jan
Masheikh: Maaskofu msiingilie mchakato wa mahakama ya kadhi
Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, imepinga tamko la maaskofu kuhusu kuzuia kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kusema hatua hiyo ni sawa na kuingilia uhuru wa Bunge.
Kutokana na hali hiyo, wametaka maaskofu hao kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), kuwaacha wabunge ili waweze kujadili muswada huo kwa uhuru bila kuwapo shinikizo katika suala hilo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka,...
10 years ago
Mwananchi25 Mar
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ni ya kibaguzi?
10 years ago
Mtanzania05 Sep
Mahakama ya Kadhi yazikwa
![Samia Hassan Suluhu](http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/06/Samia-Hassan-Suluhu.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan
Rachel Mrisho, Dodoma
SUALA la Mahakama ya Kadhi ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba na kuundiwa kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, limezikwa rasmi.
Hali hiyo imejidhihirisha jana kutokana na kutozungumziwa katika uwasilishaji wa maoni ya walio wengi, wakati kamati hizo zikiwasilisha maoni yake juu ya sura ya tisa na 10.
Imedaiwa...
10 years ago
Mwananchi19 Jan
Mahakama ya Kadhi Utata
10 years ago
Habarileo30 Mar
Wabunge wavurugana Mahakama ya Kadhi
BAADA ya kutokea kutoelewana miongoni mwa wabunge juu ya marekebisho ya muswada wa sheria inayoruhusu kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuna haja ya Serikali kutafakari upya kuhusu suala hilo kabla ya kuliwasilisha bungeni.
10 years ago
Habarileo08 Feb
Mahakama ya Kadhi yasogezwa mbele
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameeleza sababu za Bunge kushindwa kujadili miswada kadhaa, ikiwemo uliohusu Marekebisho ya Sheria ya Kiislamu, inayotambua Mahakama ya Kadhi.
10 years ago
Habarileo30 Sep
Mahakama ya Kadhi yaleta maridhiano
HOFU ya Mahakama ya Kadhi, kugawa Bunge Maalumu la Katiba na kusababisha kukwama kwa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa, imeondoka jana na kugeuka kiunganishi cha kurahisisha upitishwaji wa Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa.
10 years ago
Habarileo12 Mar
Mahakama ya Kadhi yarejeshwa bungeni
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali, likiwemo suala la Mahakama ya Kadhi, utawasilishwa katika Bunge lijalo ukiwa na maudhui ya kuangalia jinsi ya kuendesha masuala ya imani ya dini ya Kiislamu.
11 years ago
Tanzania Daima20 Mar
Waislamu walilia Mahakama ya Kadhi
JUMUIYA na taasisi za Kiislamu nchini zimeshangazwa kutokana na baadhi ya mapendekezo yao kutokuwamo kwenye rasimu ya pili ya Katiba. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,...