Masheikh: Maaskofu msiingilie mchakato wa mahakama ya kadhi
Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, imepinga tamko la maaskofu kuhusu kuzuia kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kusema hatua hiyo ni sawa na kuingilia uhuru wa Bunge.
Kutokana na hali hiyo, wametaka maaskofu hao kupitia Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF), kuwaacha wabunge ili waweze kujadili muswada huo kwa uhuru bila kuwapo shinikizo katika suala hilo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka,...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mtanzania28 Jan
Masheikh waja juu Mahakama ya Kadhi
Na WAANDISHI WETU
VIONGOZI wa dini ya Kiislamu wamepinga tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo kuhusu sheria hiyo ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kudai kuwa matamko ya aina hiyo yanaweza kusababisha machafuko nchini.
Kauli hiyo zimekuja siku moja baada ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) kutoa waraka, likipinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni wakati wowote.
Akizungumza na MTANZANIA Imamu wa Msikiti wa Idrisa uliopo Kariakoo, jijini...
10 years ago
Mtanzania27 Jan
Maaskofu:Mahakama ya Kadhi ya Kibaguzi
JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF) limepinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, likiitaka Serikali iuondoe bungeni kwa madai kuwa ni wa kibaguzi na upo kinyume na matakwa ya Katiba.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014, unapendekeza pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ya mwaka 1964.
Maaskofu na wajumbe wa jukwaa hilo walikutana Januari 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushauri Serikali iondoe muswada huo bungeni...
10 years ago
Mwananchi14 Sep
Suala la Mahakama ya Kadhi katika Mchakato wa Katiba Mpya
11 years ago
Mwananchi09 Jul
Sitta ateua masheikh, maaskofu kuwarejesha Ukawa bungeni
10 years ago
Mwananchi29 Jan
Masheikh wataka maaskofu waliache Bunge lifanye kazi
11 years ago
CloudsFM09 Jul
Sitta ateua masheikh, maaskofu kuwarejesha Ukawa bungeni
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ameanza mkakati mpya wa kunusuru mchakato wa Katiba Mpya kwa kuitisha kikao cha wajumbe 27 wa Kamati ya Mashauriano ili kuondoa mpasuko kati ya wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wajumbe wengine.
Katika wajumbe hao wamo maaskofu wawili na masheikh wawili ambao Sitta amewateua kutoka katika Bunge la Katiba.
Sitta ameitisha kikao hicho jijini Dar es Salaam Julai 24 wakati kukiwa na matamko tofauti kuhusu mustakabali wa katiba...
10 years ago
Mtanzania05 Sep
Mahakama ya Kadhi yazikwa
![Samia Hassan Suluhu](http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/06/Samia-Hassan-Suluhu.jpg)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan
Rachel Mrisho, Dodoma
SUALA la Mahakama ya Kadhi ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba na kuundiwa kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, limezikwa rasmi.
Hali hiyo imejidhihirisha jana kutokana na kutozungumziwa katika uwasilishaji wa maoni ya walio wengi, wakati kamati hizo zikiwasilisha maoni yake juu ya sura ya tisa na 10.
Imedaiwa...
10 years ago
Mwananchi19 Jan
Mahakama ya Kadhi Utata
10 years ago
Habarileo28 Aug
Mahakama ya Kadhi yawekwa kiporo
SUALA la Mahakama ya Kadhi limeleta mjadala mkali katika majadiliano na wabunge wameamua suala hilo lisiingizwe kwenye Katiba. Mjadala huo mkali uliibuka katika Kamati namba Saba ilipojadili sura ya Nne ya kwenye rasimu hiyo inayozungumzia juu ya uhuru wa imani ya dini ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Ngwilizi alisema baada ya mjadala mkali wamekubaliana kutoingizwa kwenye Katiba.