Mahakama ya Kadhi yawagawa wabunge
MAHAKAMA ya Kadhi imetikisa mjadala wa Bunge Maalumu la Katiba jana. Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa idadi kubwa ya wajumbe ambao walipata fursa ya kuchangia waliendelea kuwashawishi wenzao wakubali mahakama hiyo iingizwe kwenye Katiba kwani ni chombo muhimu kwa waumini wa dini ya Kiislamu.
habarileo
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mtanzania30 Mar
Mahakama ya Kadhi yawavuruga wabunge
Na Debora Sanja na Fredy Azzah, Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana nusura wazichape kavukavu baada ya kutofautiana juu ya uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Hali hiyo ilijitokeza wakati wabunge hao wakiwa katika semina iliyohusu Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali, ambapo miongoni mwa sheria zilizomo ndani yake ni pamoja na ile ya Mahakama ya Kadhi.
Sakati hilo lilitokea katika semina kuhusu muswada huo unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni keshokutwa...
10 years ago
Habarileo30 Mar
Wabunge wavurugana Mahakama ya Kadhi
BAADA ya kutokea kutoelewana miongoni mwa wabunge juu ya marekebisho ya muswada wa sheria inayoruhusu kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuna haja ya Serikali kutafakari upya kuhusu suala hilo kabla ya kuliwasilisha bungeni.
10 years ago
Mwananchi28 Jan
Wabunge wawe wamoja mijadala kuhusu Ripoti ya CAG, Mahakama ya Kadhi
10 years ago
Mtanzania12 Jun
Bajeti yawagawa wabunge
BAJETI Kuu ya Serikali iliyosomwa jana na Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, imewagawa wabunge ambapo baadhi wameiponda, huku wengine wakiisifia.
Baadhi ya wabunge hao wakiwamo wa vyama vya upinzani na chama tawala CCM, walisema bajeti hiyo haina jambo jipya na imezidi kuongeza mzigo wa umasikini kwa wananchi.
LUHAGA MPINA
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alisema kupandisha ushuru wa mafuta ya taa, petroli na dizeli ni kuongeza ugumu wa maisha kwa mwananchi kwa sababu ongezeko lolote...
11 years ago
Mtanzania05 Sep
Mahakama ya Kadhi yazikwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan
Rachel Mrisho, Dodoma
SUALA la Mahakama ya Kadhi ambalo lilizua mjadala mkali kwenye Kamati za Bunge la Bunge Maalumu la Katiba na kuundiwa kamati ndogo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hasan, limezikwa rasmi.
Hali hiyo imejidhihirisha jana kutokana na kutozungumziwa katika uwasilishaji wa maoni ya walio wengi, wakati kamati hizo zikiwasilisha maoni yake juu ya sura ya tisa na 10.
Imedaiwa...
10 years ago
Mwananchi19 Jan
Mahakama ya Kadhi Utata
10 years ago
Habarileo08 Feb
Mahakama ya Kadhi yasogezwa mbele
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameeleza sababu za Bunge kushindwa kujadili miswada kadhaa, ikiwemo uliohusu Marekebisho ya Sheria ya Kiislamu, inayotambua Mahakama ya Kadhi.
10 years ago
Mtanzania27 Jan
Maaskofu:Mahakama ya Kadhi ya Kibaguzi
JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF) limepinga muswada unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi, likiitaka Serikali iuondoe bungeni kwa madai kuwa ni wa kibaguzi na upo kinyume na matakwa ya Katiba.
Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014, unapendekeza pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ya mwaka 1964.
Maaskofu na wajumbe wa jukwaa hilo walikutana Januari 20, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kushauri Serikali iondoe muswada huo bungeni...
11 years ago
Habarileo30 Sep
Mahakama ya Kadhi yaleta maridhiano
HOFU ya Mahakama ya Kadhi, kugawa Bunge Maalumu la Katiba na kusababisha kukwama kwa upatikanaji wa Katiba Inayopendekezwa, imeondoka jana na kugeuka kiunganishi cha kurahisisha upitishwaji wa Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa.