Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Makontena yaliyokwepa kodi zafika 2,431

IMGS3818NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amefanya tena ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kubaini kuwa idadi ya makontena yaliyotolewa bila kulipa kodi ya Serikali yamefika 2,431.

Novemba 27, Majaliwa alifanya ziara kama hiyo bandarini hapo na kubaini kuwapo makontena 349 yaliyotoroshwa bila kulipiwa kodi.

Mbali na hilo, alimtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Hebel Mhanga, hadi kufikia jana saa 11 jioni, kumpelekea ofisini kwake majina ya watumishi wote...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Habarileo

Makontena yaliyokwepa kodi yazidi kuongezeka

MAKONTENA yaliyotolewa bila kulipa ushuru katika bandari ya Dar es Salaam yamezidi kuongezeka tangu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipobaini kutoroshwa kwa makontena 2,431 katika bandari hiyo bila kulipa ushuru. Jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova, alipozungumza na waandishi wa habari, alitaja idadi mpya ya makontena hayo iliyobainika katika uchunguzi unaoendelea, yamefikia 2,489, sawa na ongezeko la makontena mapya 58.

 

9 years ago

Mwananchi

Sakata la makontena 2,431 laibua mazito

Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (Taffa), kimedai kuwa ‘mchezo’ wa kutoa makontena 2,431 bandarini bila kulipiwa tozo ya utumiaji wa bandari umefanywa na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadhi ya wafanyakazi wa benki za CRDB na NMB zenye mikataba na mamlaka hiyo.

 

9 years ago

StarTV

Ziara Ya Waziri Mkuu TPA akuta Makontena mengine 2,431 yamepotea.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi kumi wa Mamlaka ya Bandari nchini TPA kupisha uchunguzi wa upotevu wa makontena 2,431 yaliyopita chini ya Mamlaka ya Bandari bila kulipiwa kodi kati ya Machi na Septemba mwaka 2014.

Hatua hii inakuja baada ya ziara ya ghafla ya Waziri Mkuu bandarini ambapo amezungukia idara mbalimbali.

Pamoja na hatua hiyo Waziri Mkuu ametaka majina ya vigogo waliohusika na uondoshwaji wa makontena hayo kumfikia kabla ya saa kumi na moja jioni ya...

 

9 years ago

Habarileo

JK: Sijawahi kusamehe kodi makontena

RAIS mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema katika uongozi wake wa miaka 10, hakuwahi kuagiza mtu asamehewe kontena lake lisilipe kodi na angefanya hivyo, mapato ya Serikali yasingeongezeka kutoka Sh bilioni 177 kwa mwezi mpaka Sh bilioni 900.

 

9 years ago

Bongo5

Hawajakoma bado: Makontena mengine 2431 yapita bandarini bila kulipiwa kodi

4

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la reli Tanzania(TRL).

4

Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

3

Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu...

 

9 years ago

Dewji Blog

Waziri Mkuu atinga tena bandarini na TRL, akuta makontena 2431 yametoka bila kulipiwa kodi!!

IMGS3737

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar s salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.

Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa...

 

9 years ago

Michuzi

WAZIRI MKUU AVAMIA TENA BANDARINI NA TRL,AKUTA MAKONTENA 2431 YEMETOKA BILA KULIPIWA KODI.

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam  Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015  kutaka kujua ukweli wa tuhuma za...

 

9 years ago

MillardAyo

TRA ya Rais Magufuli imevunja rekodi hii makusanyo ya Kodi, yale makontena je? Hii hapa yote..

Mipango ya Rais Magufuli kuendelea kupambana na wabadhirifu wa mapato ya Serikali pamoja na zile jitihada za kuhakikisha Tanzania inakuwa na makusanyo mazuri ya mapato ya Serikali imekuja na good news leo January 06 2016. Waziri mpya wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango aliwahi kunukuliwa akisema ni aibu kwa kiongozi wa nchi kwenda nje ya […]

The post TRA ya Rais Magufuli imevunja rekodi hii makusanyo ya Kodi, yale makontena je? Hii hapa yote.. appeared first on TZA_MillardAyo.

 

9 years ago

MillardAyo

Matatu kutoka TRA >>>makusanyo ya kodi yaliyofikiwa, usajili wa pikipiki, walioshindwa kulipa kodi…

Mipango ya Rais Magufuli kuendelea kupambana na wabadhirifu wa mapato ya Serikali yameendeela kuchukua sura mpya. Kupitia Mamlaka ya Mapato TRA Rais aliweza kufanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa watendaji ambao walihusika katika upotevu wa fedha za umma pamoja na kuwabana wakwepa kodi ambao ni wafanyabiashara wakubwa. Kingine kilichonifikia leo kutoa  kutoka kwa […]

The post Matatu kutoka TRA >>>makusanyo ya kodi yaliyofikiwa, usajili wa pikipiki, walioshindwa kulipa kodi…...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani