MBARONI WAKIHUSISHWA NA MAUAJI YA WANAWAKE DAR
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya utekaji, unyanyasaji wa kijinsia na mauaji ya wanawake.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Suleiman Kova alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema watuhumiwa hao wamehusishwa na vitendo hivyo baada ya upelelezi wa kina na wa kitaalamu uliosaidia kuwakamata wahalifu hao wakiwa na vielelezo mbalimbali.
Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni...
CloudsFM
Habari Zinazoendana
11 years ago
Habarileo25 May
Sita mbaroni wakihusishwa kuongoza `Mbwa Mwitu’ Dar
JESHI la Polisi limewakamata watu 6, wanaosadikiwa kuwa ni vinara wa vikundi hatari vya `Mbwa Mwitu’, `Watoto wa Mbwa’ au `Panya Road’ . Vikundi hivyo vinajihusisha na matukio ya kihalifu jijini Dar es Salaam.
11 years ago
Uhuru Newspaper01 Jul
Wawili mbaroni kwa mauaji ya sista Dar
EVA MBESELE NA RACHEL KYALA
JESHI la Polisi limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuhusika na kifo cha Mtawa wa Kanisa Katoliki, Clesencia Kapuri (50) aliyeuawa Juni 23, mwaka huu, huko Ubungo Kibangu, Dar es Salaam.
Majambazi hao licha ya kuhusishwa na tukio hilo na kupora sh. milioni 20, pia walikuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za tukio la uporaji wa fedha katika benki ya Barclays tawi la Kinondoni.
Hata hivyo, kinara wa ujambazi katika tukio la uporaji kwenye benki hiyo,...
10 years ago
Michuzi![](http://2.bp.blogspot.com/-lTzV_oHerZc/VZGnnfjFFOI/AAAAAAAHlwk/4dx55ce0HCY/s72-c/image061%2B%25281%2529.jpg)
WATATU WATIWA MBARONI JIJII DAR ES SALAAM KWA TUHUMA ZA MAUAJI
![](http://2.bp.blogspot.com/-lTzV_oHerZc/VZGnnfjFFOI/AAAAAAAHlwk/4dx55ce0HCY/s400/image061%2B%25281%2529.jpg)
Mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa za mchana mtoa taarifa alifika kituo cha Polisi na kueleza kwamba marehemu ANNA D/O MIZINGI aliondoka tangu tarehe 26/12/2014 majira ya saa 1:00hrs...
10 years ago
StarTV03 Dec
Polisi Dar yashikilia watuhumiwa wa mauaji ya wanawake.
Na Immaculate Kilulya,
Dar Es Salaam.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam linawashikilia watu wawili kwa makosa ya mauaji ya wanawake 11 baada ya kuwarubuni kimapenzi, kuwatilia dawa kwenye vinywaji na kisha kuwateka, kuwanyanyasa kijinsia na hatimaye kuwaua.
Watuhumiwa hao ambao ni Abubakar Aman na Ezekiel Kasenegala wamekiri kuhusika na mauaji ya aina hiyo katika kipindi cha miaka miwili yakiwemo mauaji ya hivi karibuni ya wasichana wawili wa Chuo cha Ukutubi Bagamoyo mkoani...
11 years ago
Mwananchi17 Dec
Saba mbaroni mauaji ya Mabina
9 years ago
Mwananchi16 Nov
Wanne mbaroni mauaji ya kigogo Chadema
10 years ago
Habarileo05 Feb
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu akiwemo mwanamke ambao wote ni wakazi wa Kijiji cha Mkindo wilayani Mvomero mkoani hapa kwa tuhuma za mauaji ya Huruma Naloloi (32) mkazi wa Mikocheni, Kata ya Dakawa kwa kutumia bunduki na kumpora pikipiki yake.
11 years ago
Tanzania Daima28 May
Saba Tabora mbaroni mauaji ya polisi
JESHI la Polisi mkoani Tabora, linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kumuua askari polisi wawili mwishoni mwa Aprili katika eneo la Ussoke, wilayani Urambo wakati wa tukio la ujambazi. Kamanda...
10 years ago
Mtanzania02 Mar
Kigogo mbaroni kwa mauaji ya albino
NA PETER FABIAN, MWANZA
KIONGOZI wa chama kimoja cha siasa mkoani Mwanza (jina tunalo) anashikiliwa na Jeshi la Polisi akihusishwa na uhalifu wa utengenezaji wa noti bandia, utekaji na mauaji ya albino katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa.
Habari za uhakika zilizolifikia MTANZANIA kutoka vyanzo vyetu vya habari zimesema kuwa kigogo huyo alikamatwa wilayani Magu Februari 26, mwaka huu saa 7:00 usiku.
Kigogo huyo ambaye anadaiwa kuhusishwa na utekaji wa mauaji ya albino alikamatwa baada...