Mwanamuziki Papa Wemba Awasili Dar, Aelekea Bagamoyo Kunogesha Tamasha la Karibu Music Festival 2015
MWANAMUZIKI nguli wa ndansi kutoka nchini Congo (DRC) Papa Wemba amewasili usiku huu jijini Dar es Salaam tayari kwa kutumbuiza katika tamasha la Karibu Music Festival 2015.
Papa Wemba ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere (JNIA) majira ya saa nane kasoro na ndege ya shirika la Kenya (Kenya Airways-KQ).
Mara baada ya kuwasili msanii huyo pamoja na wanamuziki wake walipokewa na Meneja wake anayeratibu safari hiyo, Chebli Msaidie pamoja na waandaaji wa Tamasha...
Michuzi
Habari Zinazoendana
9 years ago
Dewji Blog07 Nov
Papa Wemba awasili Dar, aelekea Bagamoyo kwenye Tamasha la Karibu Music Festival 2015
9 years ago
Mtanzania16 Nov
Papa Wemba: Karibu Music Festival ni tamasha la kipekee
Na Hassan Bumbuli
TAMASHA la Karibu Music Festival lililomalizika hivi karibuni mjini Bagamoyo limeacha kumbukumbu ya mambo mengi kwa wapenzi wa sanaa ya muziki hapa nchini. Licha ya kwamba ni tamasha changa, lakini hakuna mtu anayeweza kufirikia kwamba ilikuwa ni mara ya pili kwa tamasha hilo kufanyika kutokana na jinsi lilivyoandaliwa kwa ufanisi mkubwa.
Mbali na maandalizi mazuri, lakini ubora wa kazi za sanaa zilizoonyeshwa jukwaani na wanamuziki mbalimbali ni sehemu ya mambo...
9 years ago
MichuziPAPA WEMBA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVAL NOVEMBA 6-8 MWAKA HUU
9 years ago
Mtanzania04 Nov
Papa Wemba kunogesha Karibu Festival kesho kutwa
NA FESTO POLEA
TAMASHA la Karibu Music Festival 2015, litazinduliwa Novemba 6 hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo, huku mwanamuziki kutoka Congo, Papa Wemba, akitarajiwa kulinogesha.
Katika Tamasha hilo lenye lengo la kukuza muziki wa Afrika, wasanii wa bongo fleva, wasanii na vikundi vya ngoma na nyimbo za asili watatumbuiza, lakini pia warsha za mafunzo mbalimbali kuhusu sanaa zitaendeshwa.
Baadhi ya wasanii wanaotarajiwa kutoa burudani ya kutosha katika siku tatu za...
9 years ago
Dewji Blog20 Oct
Nguli wa muziki Papa Wemba kutumbuiza Tamasha la Karibu Music Festival Novemba 6-8 mwaka huu
Ofisa Mauzo wa Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO), Ernest Biseko katikati ambao ni waratibu wa Tamasha la Karibu Music Festival akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. kushoto ni ni msanii, Jhikolabwino Manyika – Jhikoman na Meneja Uvumbuzi wa kinywaji cha Jebel cha Kampuni ya SBL, Attu Mynah
MWANAMUZIKI nguli wa dansi kutoka nchini Congo DR, Papa Wemba ni miongoni mwa wasanii wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la ‘Karibu...
9 years ago
Dewji Blog08 Nov
KARIBU MUSIC FESTIVALS 2015: Papa Wemba afanya maajabu Bagamoyo!
Mwanamuziki nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[BAGAMOYO-TANZANIA] Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha...
9 years ago
Mtanzania09 Nov
Papa Wemba, Weusi wafunga kazi Karibu Music Festival
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
MWANAMUZIKI nguli wa rhumba kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jules Shungu Kikumba maarufu kama Papa Wemba na kundi la muziki wa hip hop la Weusi, juzi walifunga kazi kwa shoo zao kabambe kwenye tamasha la pili la Karibu Music Festival.
Tamasha hilo la siku tatu juzi lilishuhudia maonyesho makali kutoka kwa bendi mbalimbali zilizopanda jukwaani huku Papa Wemba na Weusi wao wakiwa wa mwisho kutumbuiza usiku huo.
Papa Wemba aliwapagawisha...
9 years ago
Dewji Blog30 Oct
Mwanamuziki wa Afrika Kusini Bo Denim ‘Bo’ kutumbuiza Tamasha la Karibu Music Festival 2015
Na Andrew Chale, Modewjiblog
Mwanamuziki nyota wa na balozi wa kutetea haki za watoto nchini Afrika Kusini Bo Denim ‘Bo’ kutoka Afrika Kusini ametajwa kuwa miongoni mwa wasanii wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la ‘Karibu Music Festival’ linaloratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tamasha hilo, Amarido Charles kupitia kurasa zake za mitandao ya...
9 years ago
Bongo502 Nov
Papa Wemba kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Karibu, Bagamoyo, Nov 6
![papa-wemba](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/11/papa-wemba-94x94.jpg)