Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Rasimu ya Katiba inavyowagawa viongozi SMZ

Tangu kutoka bungeni kwa Kundi la Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananachi (Ukawa) kwenye Bunge la Katiba kwa madai ya kuchoshwa kwao na matusi, kejeli na ubaguzi, kumeibuka mijadala mikali, huku mawaziri na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa chama tawala CCM, wakivunja ukimya na kuamua kupambana na umoja huo kwa hoja kwenye hadhara.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

JAJI MKUU MSTAAFU RAYMOND MWAIKASU APENDEKEZA VIONGOZI WA JESHI LA MAGEREZA WAINGIZWE KWENYE RASIMU YA KATIBA

JAJI mkuu mstaafu Raymond Mwaikasu amependekeza Viongozi wa jeshi la magereza waingizwe  katika rasimu ya katiba kwa sababu ni watekelezaji wa sheria za nchi  husika   hivyo viongozi wakuu wa magereza washirikishe katika kamati ya ulinzi na usalama wa taifa kwa sababu ni sehemu ya nchi washirika.
Akizungumza katika warsha iliyofanyika  mjini Iringa yenye lengo la kuwajengea  uelewa wa katiba pamoja na mchakato wa marekebisho ya katiba kwa wananchi waishio wilaya ya Iringa vijijini, ...

 

10 years ago

Habarileo

SMZ yaikubali Rasimu mpya

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeelezea kuridhika na sehemu kubwa ya Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, kutokana na kuweka sawa mambo yenye maslahi kwa Zanzibar. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia hatua ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujitoa katika Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba.

 

10 years ago

Mwananchi

Viongozi SMZ, wanasheria wagawanyika

>VIongozi  wa kisiasa na wanasheria wamegawanyika visiwani Zanzibar kufuatia uamuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ), Othman Masoud Othman kuamua kujiuzulu katika kamati ya kuandika Katiba Mpya  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

10 years ago

Michuzi

Bunge Maalum la Katiba laanza mijadala ya Rasimu ya Katiba rasmi leo

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 9 Septemba, 2014 limeanza kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati mbalimbali zikiwemo Kamati namba Kumi na Mbili, Kamati namba Mbili, Kamati namba Moja, Kamati namba Nne, Kamati namba Nane, Kamati namba Tano, Kamati namba Tisa, Kamati namba Tatu, Kamati namba Sita pamoja na Kamati namba Kumi na Moja.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge hilo ni pamoja suala la baadhi ya viongozi kumiliki akaunti zao za fedha...

 

10 years ago

Mwananchi

Madaraka ya Bunge sasa, katika Rasimu ya Katiba Mpya na Katiba inayopendekezwa

Natambua kwamba bado tuna joto la sakata la “escrow” ambalo hata baada ya Mkuu wa Nchi Rais Jakaya Kikwete kulifafanua na hata kama hujui kusoma upepo kiasi gani utakuwa umegundua na utaungana nami kwamba bado wananchi wamegawika kabisa.

 

10 years ago

GPL

MH. CHENGE AWASILISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta (kushoto) Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo. Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni siku ya kesho. Makabidhiano yakiendelea.… ...

 

11 years ago

Michuzi

HARAKATI ZA BUNGE LA KATIBA: WANAWAKE NA RASIMU YA KATIBA MPYA

Je, rasimu ya Katiba mpya imeongeza nini na imepunguza nini katika kumkomboa mwanamke? Msikilize hapa Profesa Ruth Meena akizungumzia jinsi mwanamke alivyopewa kipaumbele katika rasimu hii na ameelezea kundi gani limezungumziwa na kuongezwa kwenye rasimu hii ambayo imesahau makundi kama watoto wa kike, wazee na kusahau wanaathirika vipi katika jamii yetu ya Tanzania. Pia, amegusia kuwa nchi hii ina rasilimali nyingi zinazoweza kumlinda mwanamke na vizazi vyake. 
 Tazama video hapa...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani