Shahidi aeleza trafiki feki alivyofukuzwa chuoni
SHAHIDI wa pili katika kesi ya aliyejifanya askari polisi wa usalama barabarani, James Hassan (45) ameileza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa mshitakiwa huyo alifukuzwa baada ya kuchelewa kuingia chuoni.
habarileo
Habari Zinazoendana
10 years ago
Uhuru Newspaper14 Aug
Shahidi aeleza trafiki feki alivyopata sare za polisi
NA SYLVIA SEBASTIAN
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imeelezwa kuwa mshitakiwa James Hassan (45), anayedaiwa kujifanya askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, alijipatia kofia na mkanda baada ya kufa kwa baba yake mdogo na kisha kushona sare za kikosi hicho.
Koplo Julius (36), ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa Jamhuri, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, alipokuwa akitoa ushahidi.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Felista Mosha, Koplo Julius alidai Agosti 14,...
11 years ago
Habarileo17 Jul
Shahidi aeleza watuhumiwa walivyokamatwa
SHAHIDI wa tatu wa kesi ya wizi wa simu za thamani ya Sh milioni 19.4 inayowakabili wafanyakazi sita wa Kampuni ya kupakia na kupakua mizigo ya Swissport, ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa aliwakamata watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti.
9 years ago
Habarileo10 Dec
Shahidi aeleza Mwale ‘alivyocheza’ na akaunti
SHAHIDI wa kwanza katika kesi inayomkabili wakili maarufu hapa, Median Mwale na wenzake watatu, Ofisa wa Jeshi la Polisi, Fadhili Mdem, ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kuwa Mwale alipokea dola za Marekani kutoka akaunti ya Moyale Precious Gems Mineral and Enterprise Ltd iliyofunguliwa ikiwa na upungufu wa nyaraka.
10 years ago
Habarileo28 Aug
Shahidi aeleza alivyoingiliwa kimwili na mganga
SHAHIDI wa pili katika kesi ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu inayomkabili mganga wa kienyeji, Yahaya Michael (34) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi alivyoingiliwa kimwili na mganga huyo kwa madai kwamba atampatia dawa ya kupata mtoto.
11 years ago
Mwananchi02 Apr
Shahidi aeleza alivyoshuhudia uporaji Mwanga
11 years ago
CloudsFM05 Aug
TRAFIKI ‘FEKI’ AIBUA MAZITO
SAKATA la askari 'feki' wa Kikosi cha Usalama Barabarani, kunaswa wakiwa na sare za jeshi hilo baada ya kufukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali, bado limeendelea kulitesa Jeshi la Polisi nchini. Agosti 14,2013, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, lilimkamata 'Trafiki feki', aliyefahamika kwa jina la James Hussein (45), mkazi wa Kimara Tangibovu, katika eneo la Tabata, Kinyerezi akijifanya askari wa kikosi hicho.
Juzi katika eneo la Chamazi Muhimbili, askari mwingine 'feki'...
10 years ago
Habarileo27 Jan
Trafiki feki jela miaka 6
ALIYEJIFANYA Askari Polisi wa Usalama Barabarani, James Hassan (54) amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na sare za Polisi na kujifanya mtumishi wa jeshi hilo.
11 years ago
Tanzania Daima05 Aug
Shahidi aeleza mshitakiwa alivyosaidiwa kutorosha twiga
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Moshi, Kilimanjaro imeelezwa namna mshitakiwa namba moja katika kesi ya utoroshaji wa wanyama hai 130 wakiwamo twiga wanne kwenda nchi za Falme za Kiarabu, Kamran Ahmed,...
11 years ago
Mwananchi24 Mar
Shahidi aeleza mengi mauaji ya polisi Mwanga