Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Watengeneza noti bandia wanaswa Dar

Suleiman-Kova

 Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova.

Na Mwandishi wetu

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa  kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za Dolla milioni moja na sitini na nne  ambazo ni sawa na sh bilioni moja milioni mia saba na mbili na laki nne.

Kamanda Kova alisema tukio hilo lilitokea mnamo Agosti 4 huko  Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni.

Kova alisema polisi walipata taarifa toka kwa wasamaria wema...

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Habarileo

Matatani kwa kukutwa na noti 13 bandia

POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu sita kwa tuhuma tofauti, ikiwemo kukutwa na mali ya wizi pamoja na noti bandia. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, alisema Ahmed Msangi alisema watu hao walikamatwa katika maeneo mawili tofauti jijini hapa.

 

9 years ago

Habarileo

Wasiosikia waelimishwa kutambua noti bandia

WATU wenye ulemavu wa kutosikia mkoani Simiyu wameanza kupatiwa mafunzo na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) juu ya kutambua noti bandia na halali na njia sahihi za kutunza fedha.

 

10 years ago

Mtanzania

Noti bandia zawafikisha askari kizimbani

Na Samwel Mwanga, Simiyu
ASKARI wawili wa Jeshi la Polisi na Magereza waliokamatwa na noti bandia na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, wakikabiliwa na makosa mawili.
Washtakiwa hao ambao ni wenye namba H 2420 PC Seleman Juma (25) aliyekuwa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na B. 6499 Wdr Edmund Masaga (28) wa Gereza la Wilaya ya Bariadi, walifikishwa mahakamani hapo juzi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama...

 

10 years ago

Mwananchi

Akiri kukutwa na noti bandia Sh70,000

Mkazi wa Rumala wilayani Ilemela, Erick Godwin (21) amekiri kukutwa na fedha bandia ambazo kama zingekuwa halisi zingekuwa na thamani ya Sh70,000, lakini akadai hakuwa anafahamu lolote.

 

11 years ago

Habarileo

Watumia noti bandia kulipa wakulima wa ufuta

WAFANYABIASHARA wilayani Nachingwea mkoani Lindi wanadaiwa kutumia fedha bandia kununulia zao la ufuta.

 

10 years ago

Mtanzania

Askari aliyekutwa na noti bandia afukuzwa kazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
JESHI la Magereza nchini, limemfukuza kazi askari wake wa Gereza la Bariadi, mkoani Shinyanga kwa kosa la kupatikana na fedha za bandia kinyume cha sheria.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja, ilimtaja askari huyo kuwa ni Namba B. 6499 Wdr. Edmund Masaga.
Alisema askari huyo amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28 mwaka huu kwa kosa la kulidhalilisha jeshi hilo...

 

11 years ago

Habarileo

Polisi washikilia vijana wawili kwa noti bandia

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed MsangiPOLISI mkoani hapa inawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya Sh 285,000.

 

10 years ago

Michuzi

SABA WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA NOTI BANDIA ZA DOLA ZA KIMAREKANI WAKAMATWA

Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha noti bandia zilizokamatwaJeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani