Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Watu 2 wapoteza maisha kwenye ajali ya basi la Smart eneo la Lugoba leo asubuhi

unnamed

Basi la Smart likiwa limepinduka eneo la Lugoba.

unnamed (1)

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata mshtuko.

unnamed (2)

Watu wawili Wamefariki Dunia Kutokana na Ajali ya Basi la Smart Asubuhi ya leo.

Basi Hilo Lililokuwa likitokea Jijini dar es salaam Kuelekea Mombasa Nchini Kenya Limeacha Njia Na Kupinduka na Kusababisha Vifo vya watu Wawili pamoja na Kujeruhi abiria wanaokadiriwa kufika 20 .Ajali hiyo imetokea katika Eneo la Mkata na Lugoba  Barabara Kuu ya Chalinze...

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZZZ....: WATU ZAIDI YA 10 WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA ENEO LA MAKONGO,JIJINI DAR MCHANA HUU

 Watu zaidi ya kumi wamepoteza maisha kwenye ajali ya Daladala inayofanya safari zake kati ya Ubungo - Tegeta jijini Dar mchana huu,baada ya kushindwa maarifa ya kiudereva kwa Dereva wa daladala hilo hali iliyompelekea dereva huyo kuhama mpaka upande wa pili wa barabara na kulivaa lori kwa nyuma.Chanzo cha ajali hiyo inaelezwa kuwa ni mwendo kasi.  Hili ndilo lori lililokuwa likipita katika upande huo wa Barabara na kufatwa na daladala hiyo.

 

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MAFINGA, IRINGA, LEO BAADA YA BASI LA ABIRIA KUANGUKIWA NA KONTENA

Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo...

 

10 years ago

Michuzi

watatu wapoteza maisha katika ajali ya basi mkoani mbeya leo

Watu watatu wamepoteza maisha leo baada ya basi la abiria  liitwalo Super Feo linalofanya safari zake toka Mbeya Songea baaya ya kupata ajali maeneo ya Inyara mkoani Mbeya likiwa na abiria 20. Habari zinasema dereva wa basi hilo lenye uwezo  wa kubeba abiria 53 kutaka kulipita gari lingine  bila ya uangalifu ambapo akakutana na roli mbele yake hivyo katika kujiokoa akakimblia kulia zaidi ndipo basi likapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvati.Waliotajwa kupoteza maisha ni Anastazia...

 

10 years ago

Vijimambo

TASWILA KUTOKA ENEO LA AJALI KAHAMA BASI LA KAMPUNI YA WABONELA LILILOPINDUKA LEO ASUBUHI

Wananchi wakishuhudia basi la Wibonela lililopinduka leo asubuhi huko Kahama.Wananchi wakiwa eneo la ajali huku wengine wakijaribu kupata picha za hapa na paleWATU kadhaa wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa asubuhi hii kwenye ajali ya basi la Wibonela lililokuwa likitoka Kahama kwenda Dar lililopinduka eneo la kona ya Phantom, Kahama.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi uliopelekea dereva wa basi kushindwa kulimudu lilipofika kwenye kona ya Phantom na kupelekea kuingia mtaroni na...

 

11 years ago

Michuzi

WAWILI WAPOTEZA MAISHA NA SABA WAMEJERUHIWWA KATIKA AJALI YA BASI NA BODABODA MKOANI LINDI LEO

Watu wawili wamefariki dunia leo baada ya bodaboda yenye usajili namba T 293 ARM kugongwa na basi la abiria la kampuni ya Maning Nice lenye usajili namba T624 CQD ambalo nalo lilipinduka baada ya ajali hiyo katika kijiji cha Ngongo mkoani Lindi  na abiria saba walijeruhiwa. Majina ya marehemu na ya majeruhi hayakuweza kupatikana mara moja. Picha na Abdulaziz Video.

 

10 years ago

Vijimambo

PICHA ZINATISHA,AJALI ILIYOTOKEA USIKU WAKUAMKIA LEO HUKO NZEGA WATU 6 WAPOTEZA MAISHA

Watu 6 wamefariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya iliyohusisha magari manne huko Undomo wilayani Nzega usiku wa kuamika leo.

 

10 years ago

Dewji Blog

Wawili wapoteza maisha na 52 wajeruhiwa ajali ya basi Singida

DSC00457

Askari wa usalama barabarani wilaya ya Ikungi, akikagua basi la kampuni ya KISBO, T.534 CHX baada ya kupinduka katika eneo la kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 52.

Na Nathaniel Limu, Singida

ABIRIA wawili wamefariki dunia na wengine 52 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka.

Basi lililohusika na ajali hiyo ni T.534 CHX aina ya...

 

11 years ago

Michuzi

17 wapoteza maisha na 56 wajeruhiwa katika ajali ya basi la morobest dodoma

TAKRIBANI watu 17 wamepoteza maisha  na wengine  56  kujeruhiwa baada ya basi la la Morobest lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma leo. Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Said Lusogo liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na dereva Gilbert Isata Nemaya. Amesema atika ajali hiyo...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani