Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


WAZIRI CHIKAWE AMALIZA ZIARA YAKE JIMBONI NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akipokelewa kwa shangwe na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kipara-Mtua, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kabla ya kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo na kujua kero mbalimbali zinazowakabili viongozi hao. Aidha, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE AFUTURISHA WATOTO YATIMA JIMBONI KWAKE NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akifurahi na Watoto Yatima na Waishio katika Mazingira Hatarishi wa Kituo cha Nawoda mjini Nachingwea mkoani Lindi kabla ya kufuturu nao futari maalum aliyoiandaa kwa ajili ya watoto hao zaidi ya 80 ambao wanalelewa katika kituo hicho. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akijiandaa kufuturu na Watoto Yatima na Waishio katika...

 

11 years ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU JIMBONI KWAKE NACHINGWEA LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo...

 

10 years ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKIANA NA WAGOMBEA SERIKALI ZA MITAA KUPIGA KAMPENI YA NYUMBA KWA NYUMBA JIMBONI NACHINGWEA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Libundu, Kitongoji cha Nangote, Kata ya Kiparamnero wilayani Nachingwea katika Kampeni ya nyumba kwa nyumba ya kuwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa wilayani humo. Waziri Chikawe aliwaomba wananchi wa Nachingwea kuwapigia kura viongozi hao waliopitishwa na CCM kugombea nafasi hizo walizoomba. Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika...

 

10 years ago

Michuzi

WAZIRI MKUYA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI MAREKANI

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa CITI na Mkuu wa Afrika kwa kundi la sekta ya utumishiwa umma Bw. Peter M. Sullivan alipo mtembelea Mhe.Waziri kwa madhumuni ya kuisadia nchi ya Tanzania katika ubalozi wa Marekani mjini Washington DC. Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya wa katikati akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania walipokutana na Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki Bw.Herve’ Joly walipokuwa wakijadiliana na...

 

11 years ago

Michuzi

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI MOROGORO

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla amemaliza ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Mhe. Makalla amemaliza ziara hiyo kwa kutembelea miradi ya maji ya Halmashauri za Wilaya za Ulanga na Kilombero na kukagua utekelezaji wake.
“Utekelezaji unaenda vizuri, isipokuwa kasi iongezwe ili miradi yote ikamilike kwa wakati, na nitafuatilia kwa ukaribu miradi yote niliyoikagua na nitarudi kuangalia maendeleo yake”. Wakati umefika kuhakikisha sekta ya maji inatekeleza sera zake...

 

11 years ago

Michuzi

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI TABORA,ALA CHAKULA CHA MAMALISHE KUWAUNGA MKONO,AHITIMISHA ZIARA YAKE KWA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA/

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Stendi Kuu ya Zamani mjini Tabora, baada ya kumaliza ziara yake ya siku 11 katika mkoa huo, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata  Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi Wakazi wa Mji wa Tabora Mjini  wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye...

 

10 years ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA MNARA WA TTCL NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya TTCL katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei leo, ambapo viongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na mamia ya wananchi kutoka vijiji vilivyonufaika na mtandao huo wa mawasiliano vya Kiegei A, B, Namatunu, Nanjihi, Kilimarondo, Mbondo, Nahimba na...

 

10 years ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 22 KKKT NACHINGWEA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo....

 

10 years ago

Michuzi

WAZIRI SIMBA AMSIMIKA CHIKAWE KUWA MLEZI UWT NACHINGWEA


 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumkabidhi fimbo ya ulezi baada ya kumvalisha joho, kofia na skafu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Wapili...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani