Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


9 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA TRENI KULIGONGA BASI UTURUKI

Taswira baada ya ajali kutokea. WATU tisa wamepoteza maisha wakati watano wakijeruhiwa baada ya treni la abiria kuligonga basi dogo nchini Uturuki. Mabaki ya basi yakiwa eneo la ajali. Basi hilo lililokuwa likiwapeleka wafanyakazi eneo la viwanda mjini Mersin, limegongwa wakati likivuka reli.
Waliopoteza maisha wote walikuwa ndani ya basi dogo ambapo watu watatu kati ya majeruhi wana hali mbaya. Katika treni hakuna...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

wawili wapoteza maisha, saba wajeruhiwa na wanne hawajulikani walipo baada ya ajali ya treni ya mizigo gulwe, dodoma

Mnamo tarehe 27.03.2014 majira ya saa 02:10 usiku huko Gulwe katika Wilaya ya Mpwapwa kulitokea ajali ya treni ya mizigo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Kigoma baada ya kusombwa na mkondo wa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha. Kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo ilifanya kichwa cha treni hiyo kutumbukia kwenye mto Mimo.
                VIFO: Ajali hiyo hadi hivi sasa imesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefahamika kwa majina yafuatayo:- 1.  Felix s/o Kalonga 2.  Ismail @...

 

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: WATU ZAIDI YA 30 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA MAFINGA, IRINGA, LEO BAADA YA BASI LA ABIRIA KUANGUKIWA NA KONTENA

Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.
Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo...

 

11 years ago

Mwananchi

27 wapoteza maisha ajali za treni 2013

>Jumla ya watu 27 wamepoteza maisha yao na wengine 27 wamejeruhiwa katika matukio yanayohusisha  ajali za treni zilizotokea nchini mwaka jana.  Kamanda wa Kikosi cha Reli Tanzania, Saada Haji akizungumza na gazeti hili alisema kwamba jumla ya ajali 79 zinazohusisha treni zilitokea mwaka jana katika mikoa tofauti nchini.

 

10 years ago

Dewji Blog

Wawili wapoteza maisha na 52 wajeruhiwa ajali ya basi Singida

DSC00457

Askari wa usalama barabarani wilaya ya Ikungi, akikagua basi la kampuni ya KISBO, T.534 CHX baada ya kupinduka katika eneo la kijiji cha Kambi ya mkaa kata ya Issuna wilaya ya Ikungi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 52.

Na Nathaniel Limu, Singida

ABIRIA wawili wamefariki dunia na wengine 52 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasuka tairi la mbele kulia na kuacha barabara na kisha kupinduka.

Basi lililohusika na ajali hiyo ni T.534 CHX aina ya...

 

11 years ago

Michuzi

17 wapoteza maisha na 56 wajeruhiwa katika ajali ya basi la morobest dodoma

TAKRIBANI watu 17 wamepoteza maisha  na wengine  56  kujeruhiwa baada ya basi la la Morobest lililokuwa linatoka Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori eneo la Pandambili, Kongwa mkoani Dodoma leo. Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Said Lusogo liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na dereva Gilbert Isata Nemaya. Amesema atika ajali hiyo...

 

10 years ago

Michuzi

watatu wapoteza maisha katika ajali ya basi mkoani mbeya leo

Watu watatu wamepoteza maisha leo baada ya basi la abiria  liitwalo Super Feo linalofanya safari zake toka Mbeya Songea baaya ya kupata ajali maeneo ya Inyara mkoani Mbeya likiwa na abiria 20. Habari zinasema dereva wa basi hilo lenye uwezo  wa kubeba abiria 53 kutaka kulipita gari lingine  bila ya uangalifu ambapo akakutana na roli mbele yake hivyo katika kujiokoa akakimblia kulia zaidi ndipo basi likapinduka mara tatu na kufikia kwenye kalvati.Waliotajwa kupoteza maisha ni Anastazia...

 

11 years ago

Dewji Blog

Watu 2 wapoteza maisha kwenye ajali ya basi la Smart eneo la Lugoba leo asubuhi

unnamed

Basi la Smart likiwa limepinduka eneo la Lugoba.

unnamed (1)

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa amepoteza fahamu baada ya kupata mshtuko.

unnamed (2)

Watu wawili Wamefariki Dunia Kutokana na Ajali ya Basi la Smart Asubuhi ya leo.

Basi Hilo Lililokuwa likitokea Jijini dar es salaam Kuelekea Mombasa Nchini Kenya Limeacha Njia Na Kupinduka na Kusababisha Vifo vya watu Wawili pamoja na Kujeruhi abiria wanaokadiriwa kufika 20 .Ajali hiyo imetokea katika Eneo la Mkata na Lugoba  Barabara Kuu ya Chalinze...

 

11 years ago

Michuzi

WAWILI WAPOTEZA MAISHA NA SABA WAMEJERUHIWWA KATIKA AJALI YA BASI NA BODABODA MKOANI LINDI LEO

Watu wawili wamefariki dunia leo baada ya bodaboda yenye usajili namba T 293 ARM kugongwa na basi la abiria la kampuni ya Maning Nice lenye usajili namba T624 CQD ambalo nalo lilipinduka baada ya ajali hiyo katika kijiji cha Ngongo mkoani Lindi  na abiria saba walijeruhiwa. Majina ya marehemu na ya majeruhi hayakuweza kupatikana mara moja. Picha na Abdulaziz Video.

 

10 years ago

Vijimambo

AJALI YATOKEA MKOANI TABORA BAADA YA BASI KUGONGA TRENI

 Ajali imetokea barabara ya kwenda Urambo eneo la Mororo,Tabora ikihusisha treni na basi la abiria. Inasemekana kuna watu wamepoteza maisha kwenye eneo la tukio baada ya gari la abiria kugongana na treni la mizigo, watu waliofariki bado hajafahamika idadi yao kamili waliotambuliwa ni wawili mmoja ni Samweli mkazi wa kata ya Ufuruma wilayani Uyui na Mwingine ni Issa.
Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani