Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Abiria waharibu vifaa treni mpya

Waziri wa Uchukuzi, Samuel SittaSIKU chache baada ya kuzinduliwa kwa treni mpya ya abiria (Deluxe), abiria wa awali kutumia usafiri huo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, wamekosa ustaarabu na kufanya uharibifu katika baadhi ya mabehewa.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

ABIRIA WA TRENI MKOANI DODOMA KUTUMIKA KITUO KIDOGO CHA KATOSHO BADALA YA STESHENI YA TRENI YA KIGOMA KWA TRENI ZA ABIRIA KUANZIA FEBRUARI 18, 2015

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitka kutangaza kuwa treni za abiria za kwenda Kigoma hazitofika katika stesheni ya Kigoma badala yake zitatumia kituo kidogo cha Katosho.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya Uongozi wa TRL lilitolewa Februari 16, 2015 uamuzi wa treni  kutofika katika stesheni ya Kigoma  unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mjini  Kigoma na hivyo kuzoa mchanga ambao umefunika tuta la reli katika eneo la  stesheni ya Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo abiria wote...

 

9 years ago

Mwananchi

Treni ya mizigo yaanguka, abiria 1,000 wa treni wakwama Dodoma

Zaidi ya abiria 1,000 waliokuwa wakisafiri kwa treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mikoani ya Kigoma na Mwanza wamekwama mkoani hapa baada ya treni ya mizigo kuanguka kati ya Kituo cha Itigi na Kitalaka.

 

11 years ago

Habarileo

Abiria wa treni wamvamia RC

ZAIDI ya abiria 500 waliokuwa wakisafiri kwa treni kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam jana waliandamana hadi Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi wakitaka watafutiwe usafiri mbadala baada ya kukwama stesheni mbalimbali kwa zaidi ya siku saba.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Abiria wa treni wakwama Manyoni

ZAIDI ya abiria 700 waliokuwa wakisafiri na treni ya abiria wakitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam, wamekwama kwa siku mbili wilayani Manyoni, baada ya treni ya mizigo kuanguka. Wakizungumza na...

 

11 years ago

Habarileo

Treni ya abiria bara kuanza leo

HUDUMA ya usafiri wa treni ya abiria kuelekea bara zinaanza rasmi leo, huku, Kampuni ya Reli ya Tanzania (TRL) ikiwahakikishia wananchi kutokuwa na hofu juu ya usafiri huo.

 

10 years ago

Michuzi

MABEHEWA 22 YA TRENI YA ABIRIA YA DELUXE NI MAPYA! - TRL

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa potofu zilizoandikwa na baadhi ya magazeti kuwa mabehewa 22 ya abiria yaliyonunuliwa na Serikali kutoka Korea ya Kusini ni mabovu. Mabehewa haya yalikwisha fanyiwa majaribio na TRL kuridhika kuwa hayana kasoro yoyote.
Hoja kuwa tokea yawasili nchini mwezi Desemba , 2014 hayajaanza kutumika kwa vile ni mabovu ni upotoshaji wa ukweli. Ukweli ni kwamba kuanzia Novemba 24, 2014 TRL ilipeleka ...

 

11 years ago

Michuzi

KUSITISHWA KWA MUDA HUDUMA YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na kutetereka kwa  daraja la reli kati ya stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa  daraja utakapokamilika.
Tokea asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na...

 

10 years ago

Michuzi

Treni ya abiria imeahirishwa kuondoka hadi kesho Januari 14, 2015

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Jumanne Januari 13, 2015 saa 9 alasiri maeneo ya Stesheni ya Pugu Mpiji ambapo mabehewa matatu ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara yaliacha njia na moja kuanguka...

 

10 years ago

Michuzi

TRL YASITISHA SAFARI ZA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi  sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.
Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani