Ajali yaua 12 Iringa, 28 taabani
Abiria 12 wamefariki leo huku wengine 28 wamejeruhiwa mara baada ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori maeneo ya Igeme, Kilolo leo mchana.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mtanzania12 Mar
Ajali ya basi yaua 42 Iringa
WATU 42 wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba mbao.
Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi katika eneo la Changalawe, Mafinga mkoani Iringa.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo aliiambia MTANZANIA kwamba basi hilo namba T438 CDE, mali ya Kampuni ya Majinjah Express lilikuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo basi hilo liligongana na lori hilo lililokuwa likitoka Iringa...
9 years ago
Global Publishers18 Dec
Ajali ya basi yaua 12 na kujeruhi 22 Iringa
Taswira kutoka eneo la ajali.
Takribani watu 12 wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine 22 wakijeruhiwa baada ya basi la New Force kupata ajali leo eneo la Mahenge Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na limepata ajali mchana huu.
Jitihada za kuondoa miili na kusafirisha majeruhi kuwapeleka hospitali zinaendelea.
9 years ago
Mtanzania05 Jan
Ajali ya basi yaua wanne Iringa
Na Mwandishi Wetu, Iringa
WATU wanne wamefariki dunia katika ajali ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Luwinzo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Ajali hiyo ilitokea jana wilayani hapa kwa kuhusisha basi hilo lenye namba za usajili T 782 ACR linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es salaam ambalo lilipata ajali asubuhi katika eneo la Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa.
Basi hilo lililokuwa likisafiri kutokea Njombe kuelekea Dar es Salaam liligongana na lori lenye namba za usajilli T 718...
11 years ago
Michuzi23 Jun
NEWS ALERT:AJALI YAUA MTU MMOJA IRINGA
Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana ...
10 years ago
BBCSwahili05 Aug
Ajali:Polisi taabani kwa kudanganya Kenya
11 years ago
Tanzania Daima31 Mar
Ajali yaua 21
WATU 21 wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Mkupuka, Kibiti, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani. Watu...
11 years ago
Mtanzania31 Jul
Ajali yaua 19
![Ajali ya basi la Morobest iliyotokea mkoani Dodoma](http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/ajali-dodoma.jpg)
Ajali ya basi la Morobest iliyotokea mkoani Dodoma
Debora Sanja, Dodoma na Fadhili Athumani, Mwanga
WATU 19 wamepoteza maisha na wengine 64 wamejeruhiwa katika ajali mbili zilizotokea katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro.
Habari kutoka mkoani Dodoma zinasema watu 17 wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 2 asubuhi, katika eneo la Pandambili, lililoko Barabara ya Dodoma-Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari...
10 years ago
Habarileo16 Jun
Ajali yaua 23
WATU 23 wamekufa katika ajali iliyohusisha basi na lori mjini Mafinga, Iringa huku wengine 34 hali zao zikiwa mbaya.
10 years ago
VijimamboAJALI YAUA 12 TANGA
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali ya basi aina ya Costal lenye namba za usajili T410 BJD lililokuwa likifanya safari zake kati ya Tanga na Lushoto likiwa limepinduka baada ya kugongana na Scania lenye namba namba T645 ABJ katika kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza. (picha: Elizabeth Kilindi via Habari Mseto blog)
WATU 12 wamekufa papo hapo na wengine 19 wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria aina ya Toyota Costa inayosafiri kati ya Tanga na Lushoto...