Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


BALOZI KAMALA AKUTANA NA MWAKILISHI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA LUXEMBOURG

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masuala ya Kimataifa wa Chama cha Wafanyabiashara cha Luxembourg Bwana Jean Claude Vesque. Bwana Claude alimtembelea Balozi Kamala leo ofisini kwake Brussels. Kushoto ni Bwana Jofrey Kabakaki afisa wa masuala ya uchumi Ubalozi wa Tanzania Ubeligi.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

Balozi kamala akutana na balozi wa ubelgiji nchini tanzania

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ubelgiji Tanzania Mhe. Adam Koeler (wa pili kutoka kulia) baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya ziara ya wadau  wa sekta za  miundombinu ya bandari, reli na kilimo itakayofanyika Ubelgiji kuanzia tarehe 19-23 Mei, 2014. Kikao kimefanyika nyumbani kwa Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania.

 

9 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AAGANA VIONGOZI WA TAASISI YA WAFANYABIASHARA YA UBELIGIJI

Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa taasisi ya Wafanyabiara Ubeligiji baada ya kumaliza kikao cha kuagana nao  Brussels. Balozi Kamala anarejea Tanzania baada ya kumaliza kipindi chake cha Kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.

 

11 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA GAVANA WA HAINAUT UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika tafrija iliyoandaliwa na Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Leclercq kuwashukuru wadau wa reli na bandari kutoka Tanzania kwa kutembelea Ubelgiji. Mhe. Leclercq ameahidi kushiriki ziara ya Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Ubelgiji watakaotembelea Tanzania mwaka huu.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Mapokezi ya Hainaut huku Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Luclercq akishuhudia....

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA VIONGOZI WA KAMPUNI YA ZETES

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Zetes ya Ubelgiji Bwana Stephan Van Hoof (kulia). Kushoto ni Bwana Ronny Depoortere Makamu wa Rais wa kampuni hiyo. Viongozi hao wamemtembelea Balozi Kamala ofisini kwake Brussels kumweleza nia ya kampuni hiyo kuwekeza Tanzania.

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI WA AFRIKA WA KAMPUNI YA TE (TE Connectivity)

Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mkurugenzi wa Afrika wa kampuni ya TE (TE Connectivity) Bi. Patricia Testa kitabu kinachobainisha fursa za uwekezaji Tanzania. Bi. Patricia amemtembelea Balozi Kamala leo Ofisi kwake Brussels kumweleza mipango ya kampuni yake kuingia katika soko la Tanzania. Pamoja na mambo mengine Balozi Kamala ameishauri kampuni hiyo kushiriki ziara ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Ubelgiji itakayofanyika Tanzania mwezi Novemba...

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MEYA WA MANISPAA YA COVVIN UBELGIJI

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) amekutana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Covvin ya Ubelgiji Bwana Raymond Douniaux (kulia). Balozi Kamala amemuomba Mhe Meya huyo kutangaza Utalii wa Tanzania na amemkabidhi vifaa ya kutangaza utalii wa Tanzania.

 

10 years ago

Michuzi

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI WA KAMPUNI YA LOTUS

Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni Lotus,Bwana Matthieu Boone. alipomtembelea ofini kwake mjini Lembeke, Ubelgiji .

 

11 years ago

Michuzi

RAIS WA TERVUREN ROTARY CLUB AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Rais wa Tervuren Rotary Club Mhe. Birgit Regine Rohde akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Brussels. Mhe Birgit alimweleza Balozi Kamala uamuzi wa Tervuren Rotary Club kumtunuku nishani ya Paul Harris Bwana Ward Lernout kama ishara ya kutambua mchango wake wa kusaidia kituo cha watu wasiokia cha Msanda kilicho Mkoa wa Kilimanjaro Tanzania. Balozi Kamala amewashukuru Tervuren Rotary...

 

11 years ago

Michuzi

MKURUGENZI WA SEKRETARIETI YA DUNIA YA NISHATI AKUTANA NA BALOZI KAMALA

Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Dunia ya Nishati Bwana. Steivan Defilla (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada ya kumaliza kikao ofisini kwake. Kulia ni Bwana. Nodal Tayel Mratibu wa Taasisi hiyo. Ujumbe huo ulifika Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Brussels kueleza faida za nchi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Nishati Duniani.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani