Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


CCM kupinga matokeo majimbo manne

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimelalamikia utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo uliofanywa kwenye baadhi ya majimbo, hivyo kimekusudia kukata rufaa kupinga matokeo yaliyotangazwa kwenye majimbo manne ambayo ni Mikumi, Kawe, Iringa Mjini na Ndanda.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Habarileo

CCM kupinga mahakamani matokeo ya majimbo manne

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kutoridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye majimbo ya Kawe, Ndanda, Mikumi na Iringa Mjini na kimesema kitayapinga matokeo hayo mahakamani.

 

9 years ago

Mwananchi

MATOKEO YA AWALI: Dk Magufuli anaongoza majimbo tisa, Lowassa manne

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jioni hii imeendelea kutoa matokeo ya awali ya urais katika majimbo 13 ambapo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli anaongoza kwa majimbo tisa wakati Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa anaongoza majimbo manne.

 

9 years ago

Mtanzania

CUF kupinga matokeo ya ubunge majimbo sita

NA PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinatarajia kufungua kesi katika mahakama mbalimbali nchini kupinga matokeo ya majimbo sita katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam jana, Ofisa wa Haki za Binadamu na Sheria wa CUF, Mohamed Mluya, aliyataja majimbo hayo kuwa ni   Lindi Mjini, Newala, Mtwara Vijijini, Pangani, Mbagala na Tabora Mjini ambayo uchaguzi wake uligubikwa na dosari mbalimbali.

Alisema...

 

9 years ago

Habarileo

CCM yazoa majimbo manne Katavi

WAKATI matokeo ya Jimbo la Kavuu mkoani Katavi yakisubiriwa kutangazwa leo, tayari CCM imeshinda katika majimbo mengine manne mkoani humo.

 

9 years ago

Habarileo

Chadema yatwaa majimbo matatu, CCM manne

Mchuano mkali wa kuwania majimbo 266 ya Tanzania unaonekana ukiwa kati ya chama tawala, CCM na Chadema ambapo hadi mchana huu CCM ilikuwa imejikingia majimbo manne wakati Chadema ikijinyakulia majimbo matatu.

Kwa upande wa CCM, imejipatia majimbo ya Lindi Mjini, Mbinga Mjini, Mbinga Vijijini na Nanyamba wakati Chadema imejihakikishia ushindi katika majimbo ya Tarime Mjini, Tunduma na Buyungu.

Tutaendelea kukujulisha kulingana na matokeo unavyoyapata.

 

9 years ago

Dewji Blog

CCM walalamikia tume ya uchaguzi NEC, kufuatia kukosa majimbo manne Tanzania Bara

January

Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM, January Makamba.

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na...

 

10 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AFANYA ZIARA YA MAJIMBO MANNE LEO MKOA WA MAGHARIBI.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mkazi wa sheia ya Mbuzini,Bi.Khadija Issa Kibwana mara baada ya kuzindua mradi wa maji safi na salama katika jimbo la Mfenesini,Mkoa wa Magharini.Katika ziara hiyo ambayo ni ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010,Ndugu Kinana leo ametembelea majimbo manne likiwemo la Bububu,Mfenesini,Dole na Mtoni.Katika ziara hiyo Ndugu Kinana pia ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye.

 

9 years ago

Michuzi

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma: MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. 
Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya...

 

10 years ago

Mwananchi

CCM yatengua matokeo majimbo ya vigogo

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetengua matokeo ya kura za maoni na kuamuru kurudiwa kwa uchaguzi katika majimbo matano, baada ya kubaini kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani