Jb: Mzee wa Swaga Ndio Movie Yangu Ninayoipenda Sana Tangu Niaze Kuigiza
Mwigizaji na muongozaji wa fiamu hapa Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ ameitaja filamu ya Mzee wa Swaga kua ndio bora zaidi kati ya filamu zake zote tangu aanze kuigiza.
“Kosa la defence ...ni goli....nafasi ya 1.ndugu zangu. Tangu nianze kuigiza hii movie naipenda sanaaa....”-JB aliandika.
Wakati ya filamu ya Mzee wa Swaga ambayo imetoka mwanzoni mwa mwaka huu akiitaja kuwa namba moja, namba mbili ilikwenda kwa filamu yake ya 14 Days, tatu, Senior Bachelor , nne, DJ Ben, huku tano akiitaja...
Bongo Movies
Habari Zinazoendana
10 years ago
CloudsFM23 Jan
SHAMSA FORD:FILAMU YA ‘I HATE MY WIFE’ ILIKUWA NI NGUMU SANA KWANGU KUIGIZA,KWA SABABU YA KUIGIZA KICHAWI.
Msanii wa filamu za Kibongo,Shemsa Ford amefunguka kati ya filamu iliyompa wakati mgumu wakiwa ‘’location’ ni filamu ya I hate my wife kwani aliigiza kama mke mchawi anayemroga mumewe.
’Yaani kati ya filamu iliyonipa wakati mgumu kuigiza ni wakati naigiza filamu ya I hate my wife kutokana na kuigiza kama mchawi mshabiki walijua kuwa ndiyo tabia yangu lakini pia kuvaa uhusika wa kiuchawi ni ngumu sana’’alisema Shemsa Ford.
10 years ago
Mwananchi25 Nov
JB bonge la bwana Kufunga mwaka na ‘Mzee wa Swaga’
10 years ago
Bongo Movies26 Feb
Mzee wa Swaga: Zamaradi Amuumbua JB Kwaku-Copy na Ku-Paste!!
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu mkubwa hapa Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ hivi juzi kati amekumbana na kashfa nzito ya kugeza moja ya filamu ya kutoka India ‘Bollywood’.
Filamu ya JB inayokwenda kwa jina la Mzee wa Swaga ambayo inafanya vizuri sokon hivi sasa inadaiwa kuwa ni “Copy and Paste” ya filamu moja maarufu kutoka Bollywood inayofahamika kwa jina la "Ladies VS Ricky Bahl".
Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni...
10 years ago
Bongo Movies27 Feb
Uwanja wa Mashabiki: Saga la Ladie Vs Ricky Bahl Vs Mzee wa Swaga
Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki mitandaoni kuhusiana na SAGA la Ladies Vs Ricky Bahl Vs Mzee wa Swaga walioziona zote mbili.
Inasikitisha sana kama wasanii wetu wanaweza kufanya uhuni huu na kutuaminisha watanzania kwamba wametunga wao.
Binafsi nimeangalia muvi ya Ladie Vs Ricky Bahl mwaka 2011 na ni moja kati ya movie ya kihindi niliyoipenda kutokana na maudhui yaliyo kwenye movie hiyo.
Ricky Bahl alicheza kama Conman mtaalam aliyekuwa anawalaghai wadada mbalimbali kwa mapenzi ya dhati...
11 years ago
Bongo Movies17 Jun
Fahamu historia fupi ya mwanadada Wastara Sajuki tangu alipoanza kuigiza mpaka sasa
Historia fupi ya mwanadada wa bongo movies - Wastara Sajuki. BONYEZA HAPA kuisoma.
10 years ago
Bongo502 Sep
Picha: Wastara kuwa mpenzi wa JB ndani ya filamu mpya ‘Mzee wa Swaga’
10 years ago
Bongo Movies10 Jan
Mzee wa swaga:JB,Cassie Kabwita,Wastara,Wellu Sengo,Thea na Mike Ndani
Tegemea mzigo huu mpya unaokwenda kwajina la “Mzee wa Swage”kosa la defence...ni goli, Iliyotengenezwa na Shikamoo Mzee na Danija Jerusalem Film.
Wakali kama, JB,Cassie Kabwita,Wastara,Wellu Sengo,Thea na Mike wameshiriki kwenye filamu hii ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni na itasambazwa na kampuni ya Stesps Entertainment.
Hii sio yakukosa madau!!!
10 years ago
Bongo Movies01 Feb
JB: Jerusalem Film Company Inazidi Kupasua Anga, Mzee wa Swaga ya Someka Zambia
"Jerusalem Film Company inazidi kupasua anga....baada ya kumshirikisha msanii mkubwa sana Zambia Cassie Kabwita kwenye sinema ya MZEE WA SWAGA tumepata coverage kwenye gazeti la The Post huko Zambia Cassie akielezea sinema ya Mzee Wa Swaga...Malengo ya Jerusalem ni kujitangaza nje ya nchi tumeanza na Zambia".
"Shukrani kwa Cassie Kabwita na sasa tunajipanga kutusua Zimbabwe!!! Sinema yetu ijayo tutaifanyia Zambia Cassie akiwa mwenyeji wetu na pia tutawaleta wasanii wawili maarufu sana...
9 years ago
Mwananchi14 Nov
Bongo movie endeleeni kuigiza wenzenu wanauza