Kamati yakubali kuondoa Muswada wa Habari
Muswada wa Haki ya Kupata Habari uliokuwa usomwe, kwa mara ya pili Jumamosi wiki hii, uko kwenye hatihati baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kukubali uondolewe na kurudishwa kwa wadau kwa ajili ya kuujadili kabla ya kurudishwa tena bungeni na kusomwa.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mwananchi27 Jun
Serikali yakubali yaishe, kutojadili muswada wa habari
10 years ago
BBCSwahili21 Jun
Google sasa yakubali kuondoa picha za uchi
11 years ago
Mwananchi20 Dec
Rais asaini muswada kuondoa kodi ya simu
10 years ago
Mtanzania28 Mar
Muswada wa habari waondolewa bungeni
Na Fredy Azzah, Dodoma
HATIMAYE Serikali imekubali kuuondoa muswada wa habari na ule wa vyombo vya habari iliyopangwa kuwasilishwa kwa hati ya dharura na badala yake itasomwa kwa mara ya kwanza kisha wadau watapata nafasi ya kuijadili.
Ratiba ya awali ilionyesha kuwa Machi 31, mwaka huu Serikali ilitarajiwa kuwasilisha muswada wa Sheria ya kupata Habari wa mwaka 2015 na ule wa Vyombo vya Habari wa mwaka 2015 yote kwa hati ya dharura.
Ratiba iliyotolewa jana ilikuwa haina miswada hiyo,...
10 years ago
Habarileo27 Jun
Muswada wa habari waondolewa bungeni
SERIKALI imeondoa muswada wa Sheria ya Haki ya Upatikanaji Habari wa mwaka 2015, uliokuwa usomwe kwa mara ya pili bungeni na hivyo utasubiri hadi Bunge jipya litakapokaa, baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
10 years ago
Mtanzania17 Mar
Muswada wa habari kuwasilishwa bungeni
Na Debora Sanja, Dodoma
HATIMAYE Muswada wa Sheria ya kupata Habari na Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2015, inatarajiwa kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa 19 wa Bunge unaoanza leo mjini hapa.
Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa hati ya dharura na inakusudiwa kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mjini hapa jan,a mbali na miswada hiyo kuwasilishwa, pia miswada mingine minne inatarajiwa kuwasilishwa kwa hati ya dharura.
“Miswada...
10 years ago
Tanzania Daima08 Nov
Muswada wa habari Februari mwakani
SERIKALI imeendelea kupiga danadana kuleta bungeni muswada wa sheria ya habari na kusema itauleta Februari mwakani badala ya mkutano huu unaoendelea. Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kusini,...
10 years ago
Mtanzania29 May
Muswada wa Habari wapingwa vikali
Na Arodia Peter, Dodoma
MUSWADA wa Habari unaotarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa, umeelezwa kuwa ni kandamizi na tishio kwa usalama wa nchi.
Muswada huo umepingwa ikiwa ni siku chache baada ya Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) kuwataka wabunge wasiupitishe kwa sababu hauna maslahi kwa taifa.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Waziri Kivuli, Joseph Mbilinyi...
11 years ago
Habarileo30 May
Muswada wa vyombo vya habari waja
SERIKALI imeweka bayana kwamba itafikisha bungeni Muswada wa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari katika Bunge lijalo la kutunga sheria. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara alisema hayo bungeni jana wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka ujao wa fedha.